Raisi wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete |
MUHTASARI WA TAARIFA YA MAENDELEO YA WILAYA YA MUHEZA KWA RAIS WA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE, WAKATI WA ZIARA
YAKE
WILAYANI MUHEZA TAREHE 26 MACHI, 2014
Mheshimiwa Rais,
Kwa niaba ya viongozi wenzangu na wananchi
wa Wilaya ya Muheza, napenda nitumie nafasi hii kukukaribisha wewe pamoja na
ujumbe wako. Tunafuraha kubwa kwa kuwa leo hii upo pamoja nasi hapa Wilayani
kwetu kwani wananchi na viongozi wamekuwa na hamu kubwa ya kukuona na
kuzungumza nawe. Karibuni sana.
1.0 UTANGULIZI
Mheshimuwa Rais,
Wilaya ya Muheza ilianza mwaka 1974, ambapo
ilimegwa kutoka katika Wilaya ya Tanga. Wilaya ina ukubwa wa kilomita za mraba
1974 kati ya hizo 1,145 zinafaa kwa kwa shughuli za Kilimo na ufugaji.
Wilaya ina Tarafa 4, Kata 33, Vijiji 135
na Vitongoji 522. Wilaya ina Jimbo moja la uchanguzi na Madiwani 44 ambao wote
ni kutoka Chama Tawala. Vilevile Wilaya yetu ina Mamlaka ya Mji Mdogo wa
Muheza, mamlaka hii inaundwa na jumla ya
Kata 6.
Kwa matokeo ya
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Muheza ina wakazi wapatao
204,461 kati yao wanaume ni 100,843 (49.3%) na wanawake ni 103,618 (50.7%) na
kiwango cha ongeeko ni 1.4%. Idadi ya kaya zilizopo 47,920 zenye wastani wa
wakazi 4.3 kwa kaya.
2.0
HALI YA KIUCHUMI
2.1 HALI YA KIPATO KWA MWANANCHI
Mheshimiwa Rais,
Asilimia 90 ya wakazi hujishughulisha na shughuli za kilimo. Kipato cha mkazi wa
Muheza kwa sasa ni wastani wa Tsh 1,026,000 kwa mwaka na lengo ni kufikia
wastani wa Tsh 1,500,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2015. Pamoja na shughuli za
kilimo wakazi wa Muheza hujishughulisha na biashara, viwanda vidogovidogo vya
useremala, uashi na uhunzi.
2.2 HALI YA
MAPATO YA HALMASHAURI
2.2.1 Mapato ya Ndani bila ya fidia ya vyanzo vilivyofutwa
Ukusanyaji wa mapato ya ndani bila fidia ya vyanzo
vilivyofutwa umekuwa ukiongezeka kila mwa kutoka Tsh. 590,479,812 (2009/10)
hadi Tsh. 803,818,862 mwaka 2012/2013, kama
inavyoonekana hapa chini;
Mwaka
|
Makisio (Tsh.)
|
Makusanyo (Tsh.)
|
% ya makusanyo
|
2009/10
|
284,072,000
|
590,479,812
|
207.86
|
2010/11
|
530,450,000
|
491,908,462
|
92.73
|
2011/12
|
645,600,000
|
705,963,718
|
109.35
|
2012/13
|
591,704,000
|
803,818,862
|
135.85
|
2013/14 hadi Desemba
|
702,691,000
|
435,626,297
|
61.99
|
2.2.2 Mapato ya Ndani pamoja na fidia ya vyanzo
vilivyofutwa
Mwaka
|
Makisio (Tsh.)
|
Makusanyo (Tsh.)
|
% ya mapokezi
|
2009/10
|
803,142,000
|
947,022,362
|
117.91
|
2010/11
|
892,435,000
|
691,373,054
|
77.47
|
2011/12
|
986,836,000
|
821,509,964
|
83.25
|
2012/13
|
955,940,000
|
1,164,934,499
|
121.86
|
2013/14 hadi Desemba
|
1,015,127,000
|
500,736,639.79
|
49.33
|
2.2.3 Ruzuku
Mwaka
|
Makisio (Tsh.)
|
Makusanyo (Tsh.)
|
% ya mapokezi
|
2009/10
|
10,081,278,117
|
8,018,144,664
|
79.54
|
2010/11
|
9,951,167,000
|
10,705,601,164
|
107.58
|
2011/12
|
13,449,077,000
|
13,481,290,709
|
100.24
|
2012/13
|
15,225,199,540
|
15,637,807,089
|
102.71
|
2013/14 hadi Desemba
|
25,093,141,910
|
8,167,904,698.52
|
32.55
|
3.0
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2010
Mheshimiwa Rais ,
Wilaya yetu imeendelea kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010 ambayo kwa mujibu wa ibara 21 inalenga kuongeza kasi ya ukuzaji wa Uchumi wa Kisasa na taifa
linalojitegemea kwa kuwashirikisha na kuwawezesha kiuchumi wananchi .
Katika
Ilani ya CCM, 2010 zimo ahadi zinazohusu Wilaya ya Muheza, pia wakati wa
kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010, Mhe. Rais, alitoa ahadi mbalimbali
ambazo zimeendelea kutekelezwa katika ngazi ya Kitaifa na Kiwilaya. Hali ya
utekelezaji wa ahadi hizo imeelezwa kwenye Jedwali Na. 1.
Jedwali
Na 1: Utekelezaji wa Ahadi na Maagizo ya Mh. Rais
Na
|
Ahadi
|
Utekelezaji
|
1
|
Kutatua tatizo la maji Muheza kwa
kutekeleza mradi mkubwa utakaotoa maji kutoka mto Zigi.
|
Usanifu wa Mradi huu ulifanyika mwaka 2011 na
Kampuni ya Arab Consulting Engineers
ya Misri na gharama za mradi huu ni zilikadiriwa kuwa Tsh.13.4 billioni.
Hatua zilizochukuliwa na Serikali Kuu
(i)Uendelezaji wa Kisima kirefu cha Polisi kwa
kujenga Miundo mbinu ya kusambaza Maji
ambapo kiasi cha Shs 100,000,000 zilizotokana na Ahadi yako Mhe Rais
zilipokelewa na kufanyiwa kazi iliyokusudiwa na huduma ya maji
inanufaisha wakazi wapatao 900 wa Kata ya Genge.
Hatua zilizochukuliwa na Halmashauri
(ii) Ujenzi wa miundombinu ya maji na uchimbaji
wa visima tisa ambapo jumla ya Shs Tsh 363,461,825.28 zimetumika (Tsh. 229,000,000/= za mapato ya ndani na 134,461,825.28
kutoka Serikali Kuu
(iii)Ununuzi wa mtambo wa kuchimba visima
ulioagizwa toka Thailand ambapo jumla ya Shs. 249,140,622.54 zilizotokana na mapato ya ndani
zimetumika
(iv) Maandiko ya kutafuata fedha yameandaliwa na
kuwasilishwa kwa Taasisi za ENCODIA ya Ugiriki, ACE Consulting Engineer –
Moharram- Bakoum na EUROHNSA S.A-
Madrid
|
2
|
Kutatua matatizo ya uhaba wa ardhi Muheza kwa kufuta hati za
mashamba ya Mkonge yaliyotelekezwa muda mrefu kwa kufuata taratibu za
kisheria.
|
Halmashauri imewasilisha maombi
kwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya
Makazi ya kubatilisha hati za umiliki wa ardhi wa mashamba nane ambapo
asilimia kubwa ya mashamba haya
yamevamiwa na Wananchi Maombi haya yaliwasilishwa kwa nyakati tofauti(
2007,2009,2010 & 2012 ) .Mpaka
sasa Halmashauri inaendelea kusubiri utekelezaji wa maombi hayo hata hivyo
mashamba haya yamevamiwa na Wananchi . Uongozi wa Mkoa na Wilaya katika
kuhakikisha wananchi wa Derema waliopisha Hifadhi ya Msitu wa Amani wanapata
fidia yao ya Ardhi Mbadala waliyoahidiwa miaka kumi iliyopita ilikutana na
Wadau wa Shamba la Kibaranga na
makubaliano yamefikiwa kuwa Shamba la Mkonge Kibaranga lipimwe na kugawiwa
kwa wahanga hao wa Derema, wakulima wakubwa na wakati wa zao la Mkonge pamoja wananchi wenye uhitaji . Hadi sasa
ekari 1224 (mashamba 408) zimepimwa. Taarifa maalumu ya shamba la kibaranga
imeambatanishwa.
|
3
|
Ujenzi wa barabara ya lami kutoka Muheza
hadi Amani
|
Matengenezo ya mara kwa mara yamekuwa yakifanyika hasa sehemu
zilizokuwa korofi, hali inazidi kuimarika.
Barabara hiyo ilimetengewa fedha mwaka 2013/2014 kwa ajili ya upembuzi
yakinifu na fedha zimetolewa kazi ya
upembuzi yakinifu inaendelea.
|
4
|
Ujenzi wa bwalo shule ya Sekondari
Muheza High School ahadi ambayo uliitoa wakati wa kufungua shule hii tarehe
19/7/2008
|
Ahadi hii mpaka sasa haijatekelezwa.
|
5
|
Ununuzi wa gari la wagonjwa (ambulance)
kwa ajili ya hospitali Teule Muheza
|
Maombi maalumu ya fedha za utekelezaji wa ahadi hii yamewasilishwa
Wizara ya Fedha (Hazina) wakati wa bajeti ya mwaka 2011/12 na Wilaya imeendelea
kukumbusha kila mwaka, pia katika bajeti ya mwaka 2014/2015 maombi maalumu
yamewasilishwa tena Hazina. Mpaka sasa Ahadi hii haijatekelezwa.
|
MAAGIZO
1
|
Kujenga maabara katika shule za
Sekondari
|
Hadi sasa Halmashauri
ya wilaya ina vyumba vya maabara 8 kwa masomo ya sayansi kati ya 75
zinazohitajika,
meza za maabara
(mobile laboratory) 6 na madarasa ya
sayansi 17 (Vyumba vya sayansi) kwa shule za Serikali, ujenzi wa
maabara 67 katika shule zote za serikali upo katika hatua mbalimbali kwa kutumia fedha za Serikali na nguvu za
Wananchi.
·
7 hatua umaliziaji.
·
2 hatua ya Lenta.
·
5 Ujenzi wa Boma
·
8 hatua ya kumwaga jamvi.
·
16 msingi umekamilika
·
20 hatua ujenzi wa msingi
·
5 Maandalizi ya awali
·
6 utekelezaji haujaanza
Lengo ni kuhakikisha kuwa Shule zote za Serikali
zinakuwa na maabara tatu kwa masomo ya sayansi hadi Novemba mwaka 2014.
|
4.0 MIPANGO YA MAENDELEO YA WILAYA
Wilaya
ya Muheza kwa kushirikiana na sekta Binafsi, Vyama vya Siasa, Wadau wa
Maendeleo na Wananchi inatekeleza Mipango mbalimbali ya Kitaifa ikiwemo;
·
Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs)
·
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
·
Mpango wa Uwiano wa Maendeleo wa Miaka 5 wa Wilaya (DIDP) kuanzia mwaka
2011/12 hadi 2015/2016.
·
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TEKELEZA SASA KWA MATOKEO MAKUBWA KWA MIAKA
YA 2013/2014- 2014/2015 (BRN)
Pamoja na vipaumbele vya kitaifa katika
mpango huu, Wilaya imejiwekea vipaumbele vyake ambavyo ni;
a)
Kukuza mapato kwa mtu mmoja mmoja kutoka wastani wa Tsh. 1,026,000 kufikia
wastani wa Tsh. 1,500,000 mwaka 2015 na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka
wastani wa makusanyo ya 4% hadi 15% ya bajeti ifikapo mwaka 2015).
Mafanikio
·
Miradi
ya kuongeza kipato kwa wananchi yenye thamani ya Tsh. 2,369,027,016/= imetekelezwa
ikiwemo; ujenzi wa masoko 2, boreshaji wa kilimo cha zao la michungwa na
mahindi, ngombe bora 40 wamegawiwa kwa wananchi, vituo vya kukusanya maziwa 2
vimejengwa na mizinga ya nyuki 170 ya kisasa imesambazwa, pia mikopo ya makundi
maalumu (kinamama na vijana) ya Tsh. 70,000,000/= imetolewa.
·
Ukusanyaji
mapato umeongezeka toka Tsh. 590,479,812/= (2009/10) hadi Tsh. 803,818,862/=
(2012/13)
b)
Sekta ya Kilimo: Lengo ni kuongeza uzalishaji wa zao la mahindi na
machungwa kwa Kuongeza uzalishaji wa mahindi kutoka tani
1.8 hadi tani 2.0/ha ifikapo Julai 2014 na kuongeza uzalishaji wa machungwa
kutoka tani 10 hadi tani 12 ifikapo Julai 2015
Utekezaji kufikia malengo
·
Matumizi
ya matrekta makubwa yameongezeka kutoka 70 mwaka 2012 hadi 73 mwaka 2013 na matrekta madogo ya mkono toka toka 45 mwaka 2012 hadi 55
mwaka 2013
·
Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka toka
tani 106,593 kwa mwaka 2012 hadi tani 142,149 kwa mwaka 2013
·
Juhudi
kuogeza uzalishaji wa zao la michungwa, lita 400 za sumu ya kudhibiti inzi
waharibifu wa machungwa zimenunuliwa na 180 zimesambazwa kwa wakulima mwaka
2013
·
Wilaya inaendeleza Skimu za umwagiliaji za Misozwe, Mashewa, na Potwe ipo katika hatua
za upembuzi yakinifu. Kupitia Skimu hizo
wilaya inategemea kuongeza uzalishaji wa Mahindi na Mchele kwa tani 2,460.
c)
Sekta ya Mifugo:
Lengo ni kuongeza uzalishaji wa maziwa ya ng’ombe
kutoka wastani wa lita 6 hadi 10 kwa
ngombe kwa siku hadi ifikapo 2015
·
Utekelezaji
kufikia malengo
·
Mitamba
ya ngombe 40 imenunuliwa na kusambazwa kwa wafugaji 40 katika Tarafa za Amani
na Muheza mwaka 2013
·
Uzalishaji maziwa umeongezeka toka lita
5,525,075 mwaka 2011 hadi lita 6,456,550 kwa mwaka 2013
·
Majosho
2 ya kuogeshea ng’ombe ya Kigombe na Muungano yamekarabatiwa na yanafanya kazi
d) Sekta ya Mazingira: Lengo
kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki hapa wilayani
·
Asali
kutoka kilo 400 na kilo 5,000
ifikapo Juni 2015
·
Nta
kutoka kilo 20 hadi kilo 300 ifikapo mwaka 2015
Utekelezaji kufikia malengo
·
Mizinga
ya nyuki 170 ya kisasa na 60 ya kienyeji
imetengenezwa katika Tarafa za Amani na
Bwembwera
·
Vijiji
15 vimeanzisha hifadhi
ya misitu ya asili ambapo shughuli za utunzaji wa mazingira kampeni za upandaji
miti na uthibiti wa moto zinafanyika ambapo miche 2,300,120 imepandwa mwaka
2012 na 1,516,198 imepandwa 2013.
·
Upandaji
miti misitu ya asili ya
vijiji
e) Sekta ya Elimu
Elimu Msingi
Lengo ni:
·
Kuinua
kiwango cha ufaulu katika Mtihani wa darasa la VII kutoka (27%) (2012) hadi kufikia 65% (2013).
·
Kuinua
kiwango cha ufaulu katika Mtihani wa Darasa la IV kutoka 90% (2012) hadi (95%)
mwaka 2013.
·
Kuwa
na asilimia 100 ya wanafunzi wa darasa II – VII wanaojua Kusoma, Kuandika na
Kuhesabu (KKK).
Utekezaji kufikia malengo
·
Wilaya imehakikisha
kila shule inakuwa na Kiongozi cha Usimamizi wa shule, miundombinu muhimu ya
shule imeboreshwa, Ruzuku za uendeshaji wa shule zimetolewa, Kuandikisha
wanafunzi 6,000 wa darasa la kwanza, Kupunguza Mdondoko na utoro, kuhimiza
chakula cha mchana mashuleni.
·
Darasa la saba ufaulu umeongezeka toka 27%
(2012) hadi 66 (2013) na mtihani wa darasa la IV ufaulu umeongezeka toka 90%
(2012) hadi 96% (2013)
·
Matokeo
ya mitihani yameongezeka kwa shule zinazoingia katika kundi la ‘Green’ kutoka shule 52 (46%) katika Mock Mkoa hadi
70 (63%) katika PSLE ongezeko la shule
18 sawa na 17%.
·
Mimba
kwa wanafunzi zimepungua kutoka 4 mwaka 2012 hadi 2 mwaka 2013
·
Asilimia
ya wanafunzi wa darasa II – VII wanaojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)
imeongezeka toka 90% mwaka 2013 hadi 92% mwezi Machi 2014.
Elimu Sekondari malengo yaliyowekwa ni:
·
Kuongeza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa kidato cha pili kutoka 32% ya
mwaka 2012 hadi kufikia 86% ifikapo
mwaka 2015.
·
Kuongeza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha Nne kutoka 19% ya mwaka 2012 hadi 65% ifikapo mwaka 2015
·
Kuongeza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka 86% ya mwaka 2012
hadi kufikia 100% ifikapo mwaka 2015
Utekelezaji kufikia malengo –
- Ili kufikia malengo Wilaya imeteua walimu wakuu kwa kila shule kwa shule zilizokuwa na Kaimu wa Wakuu wa shule
- Kuimarisha usimamizi wa shule kwa kuhakikisha kila shule ina Bodi ya Shule yenye wajumbe wenye sifa na iliyo hai
- Kufanya vikao na walimu ili kufahamu matatizo yao
- Kufuatilia kwa karibu matumizi sahihi ya fedha za Ruzuku ya ‘Capitation’
- Kuhimiza na kusimamia mitihani yote ya ndani.
·
Ufaulu kidato cha pili umeongezeka toka 32%
(2012) hadi 49% (2013)
·
Ufaulu kidato cha nne umeongezeka toka 19%
(2012) hadi 36% (2013)
·
Ufaulu
kidato cha sita umeongezeka kutoka 86% mwaka 2012 hadi 89% mwaka 2013
·
Matokeo
ya mtihani wa kidato cha Nne (Upangaji wa wanafunzi kwa madaraja)
-
Kijani
imeongezeka kutoka 11 hadi 34
-
Njano
imeongezeka kutoka 470 hadi 904
-
Nyekundu
imepungua kutoka 1,745 hadi 267
f) Sekta ya Afya
Lengo ni
kuongeza idadi ya wanachama wanaojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutoka wastani wa sasa wa 17% hadi 50% ifikapo 2015
Utekelezaji Kufikia malengo.
·
Kaya
zilizojiunga na mfuko wa CHF zimeongezeka toka 1,860 mwaka 2012 hadi 7,730
mwaka 2014, kati yake Wazee ni wakiwa 4,678. Tumefikia lengo
kwa asilimia 34% ya
kaya zote 22,698 zilizolengwa
·
Idadi
ya vituo vya kutolea huduma imeongezeka kutoka 43 mwaka 2012 hadi 47 mwaka
2014.
·
Ujenzi
wa majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) katika vituo vya afya vya Mhamba na
Misalai
umekamilika na huduma za afya zinatolewa
·
Vifaa
tiba vya thamani ya sh.74,338,600 vimenunuliwa pamoja na dawa kiasi cha kutosha
zimeagizwa
kwa mfumo wa kuagiza dawa kulingana na mahitaji halisi ya kituo husika
(Integrated
Logistic System – ILS).
g) Sekta ya Maji
Malengo ya Mwaka 2013/2014
·
Kuhakisha
kwamba vijiji 7 kati ya 10 vya program vinapata maji safi na salama
·
Kujenga
vituo 66 vya kuchotea maji (DP)
·
Watu
wapatao 39,905 wanapata huduma ya maji kwa umbali usiozidi mita 400
Utekelezaji kufikia malengo
·
Miradi
4 ambayo inahudumia vijiji 6 vya Ubembe, Kisiwani Nkumba, Kibanda Nkumba, Kwemhosi, Mamboleo na
Masimbani imekamilika na vituo 40 vimejengwa ambapo watu wapatao 6,902 wanapata huduma ya Maji. Aidha miradi 3
iko katika hatua mbalimbali, vijiji vya Misongeni na Mikwamba (inakamilika
Aprili), na Kigongomawe (unakamilika Mei) ambapo jumla ya watu 4,247 watapata
huduma ya maji.
·
Upatikanaji maji vijijini umeongezeka toka 56.3%
mwaka 2011 hadi 62.2% mwaka 2013
·
Miundombinu
ya uvunaji wa maji ya mvua imejengwa katika shule za msingi 11, Sekondari 5 na
Zahanati 8. Aidha jumla ya miradi 6 ya programu ya maji vijijini inayoendelea
kujengwa ina kipengele cha ujenzi wa miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua
katika taasisi za kijamii.
h) Usimamizi na ufuatiliaji
Kamati ya Usimamizi inayongozwa na Mkuu wa
wilaya
- Mkuu wa Wilaya – Mwenyekiti
- Katibu Tawala (W) – Mjumbe
- Afisa Usalama (W) – Mjumbe
- Mwenyekiti wa Halmashauri- Mjumbe
- Mkurugenzi Mtendaji Wilaya – Katibu
- Afisa Mipango (W) - Mjumbe
Kamati ya DDU
·
Imeundwa
ina wajumbe 3 na inafanya kazi
·
Inawajibika
kwa Mkurugenzi Mtendaji (W).
Mfumo wa ufuatiliaji
- Ukaguzi -Mkurugenzi, Madiwani, Timu ya Ufuatiliaji, DDU
- Ufuatiliaji - Mkurugenzi, Madiwani, Wakuu wa Idara, Timu ya Ufuatiliaji, DDU
- Vikao - Mkurugenzi, Timu ya Ufuatiliaji, Madiwani
5.0 SEKTA
YA UZALISHAJI - (SURA YA TATU YA ILANI YA CCM MWAKA 2010)
5.1 SEKTA YA KILIMO
5.1.1 Mazao yanayolimwa
Mazao ya biashara yanayolimwa ni Machungwa, Chai
ambayo hulimwa na makampuni yanayomiliki mashamba makubwa (Estates) na wakulima wadogowadogo , mazao ya
viungo (Iliki, karafuu, Mdalasini, Pilipili manga), Miwa, Minazi, Katani,
Korosho na mazao ya chakula ni pamoja na Mahindi, Mihogo, Ndizi, maharage, Mpunga na viazi vitamu.
5.1.2 Hali ya chakula.
Katika kipindi cha mwezi Februari hali ya chakula
iliendelea kuwa ya kuridhisha katika maeneo yote ya Wilaya kutokana na kuwepo
kwa vyakula vya wanga kama mihogo na ndizi vya kutosheleza mahitaji na ziada.
Vyakula vilivyopo ni pamoja na Mahindi, Mpunga, Viazi vitamu, mikunde, ndizi na
mihogo iliyozalishwa msimu wa masika na vuli 2013.
Hadi mwishoni mwa mwezi Februari, 2014
Wilaya ilikuwa ina akiba ya chakula cha wanga kiasi cha tani 70,392 za mahindi na
mpunga/mchele ulioko ghalani kwa wakulima na wafanyabiashara na muhogo pamoja
na ndizi vinavyovunwa shambani. Mahitaji ya chakula kwa Wananchi wa Muheza ni
tani 48,509 hivyo Wilaya ina ziada ya tani 21,883 ya chakula.
Mchanganuo wa chakula kilichopo ghalani na
mashambani ni kama ifuatavyo;
Na
|
Aina ya zao
|
Kiasi (Tani)
|
1
|
Mahindi
|
13,269
|
2
|
Muhogo
|
42,398
|
3
|
Ndizi
|
14,321
|
4
|
Mchele
|
404
|
Jumla
|
70,392
|
5.1.3 Uzalishaji wa mazao ya chakula
S/N
|
ZAO
|
MWAKA 2011 (TANI)
|
MWAKA 2012 (TANI)
|
MWAKA 2013 (TANI)
|
1.
|
Mahindi
|
35,979
|
20,117
|
29,853
|
2.
|
Muhogo
|
54,283
|
50,307
|
55,436
|
3.
|
Ndizi
|
57,770
|
34,656
|
52,029
|
4.
|
Mpunga
|
5,383
|
807
|
2,922
|
1.
|
Mikunde
|
2,230
|
706
|
1,909
|
Jumla
|
155,645
|
106,593
|
142,149
|
·
Mwaka
2012 uzalishaji ulishuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
·
Uzalishaji wa mahindi umeongezeka toka tani 1,8
kwa hekta hadi 2.5 kwa hekta
5.1.4 Uzalishaji wa mazao ya biashara
S/N
|
ZAO
|
MWAKA 2011 (TANI)
|
MWAKA 2012 (TANI)
|
MWAKA 2013 (TANI)
|
1
|
Machungwa
|
79,830
|
79,930
|
80,430
|
2
|
Mazao ya viungo
|
2,760
|
2,903
|
3123
|
3
|
Nazi
|
183,590
|
183,670
|
183,715
|
JUMLA
|
266,180
|
266,503
|
267,268
|
5.1.5 Mkakati wa kuongeza kipato cha
mwananchi kupitia zao la michungwa
Katika kuongeza
uzalishaji wa zao la Machungwa ambalo ndio zao la mnyororo wa thamani kwa Wilaya yetu,
hatua zifuatazo zimechukuliwa;-
·
Mashamba darasa 12 yameanzishwa katika maeneo ya
Mamboleo, Kwakibuyu, Songa Kibaoni, Magoda, Mkuzi, Kilulu, Mtindiro, Mkinga,
Mpakani, Mkwakwani na Kwakifua
·
Kuendeleza vitalu vya miche bora ya machungwa ikiwemo
aina ya machungwa isiyo na mbegu (seedless) vilivyoko Maduma, Kilongo na Songa. Uzalishaji wa miche ni kama ifuatavyo;
-
2011/12 - miche 5,000
-
2012/13 - miche 9,000
-
2013/14 - miche 15,000
·
Kununua dawa ya kuua inzi wa machungwa na kuuza kwa
bei nafuu kupitia vyama vya wakulima wa machungwa kwa bei ya Tsh. 22,700/= kwa
lita badala ya 27,000 – 30,000/= katika maduka ya pembejeo hadi sasa lita 400
zimenunuliwa na 180 zimeuzwa.
·
Kupambana na inzi wa machungwa kwa kuweka siku
maalumu kila mwezi ya kufukia machungwa ili kuangamiza mazalia ya inzi.
·
Kujenga kituo cha kuongeza thamani ya machungwa
kwa kuyapanga kwa madaraja, kufungasha na kuhifadhi kwenye chumba cha baridi,
Tsh. 74 milioni zimetengwa kwa kazi hiyo.
·
Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Mradi
wa Muungano wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) wametoa mafunzo ya kilimo cha
kibiashara katika zao la machungwa kwa wakulima 1400 Maafisa Ugani 45.
·
Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) 4
vimeanzishwa na kuendelezwa katika maeneo yanayolima machungwa (Kata za Songa,
Kilulu, Nkumba na Mtindiro ili kuwezesha wakulima kupata mikopo yenye riba
nafuu na uhamasishaji wa uundaji wa vyama vingine zaidi umefanyika katika kata za Kwafungo na Tingeni.
5.1.5 Mkakati wa
kuongeza kipato cha mwananchi kupitia mazao ya viungo (iliki, mdalasini,
karafuu na chai)
·
Kumekuwepo na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya
viungo kila mwaka ambapo tani 2, 760 zimezalishwa mwaka 2010/11, tani 2,903
mwaka 2011/12 na tani 3,123 mwaka 2012/13, hii inatokana na bei nzuri iliyopo
hivyo kuongeza upandaji wa mazao haya
·
Wilaya kushirikiana na Jumuia ya Wakulima wa
Kilimo Hai Usambara Mashariki (JUWAKIHUMA) wametoa mafunzo ya utunzaji wa
vitalu katika vijiji 7 na wakulima 720 wamepatiwa elimu ya kilimo bora cha
viungo
·
Wakulima wa mazao ya viungo wamefanya vikao 2
kujadili kutovuna mazao kabla ya kukomaa ili kupata soko la uhakika na bei
nzuri, mikutano hiyo imewezesha pilipilimanga kuuzwa kwa bei ya Tsh. 8,500/=
kwa kilo badala ya Tsh. 6,500/=
·
Chama cha kuweka na kukopa (SACCOs) kimeanzishwa
katika kata ya Nkumba ili wakulima waweze
kupata mikopo yenye riba nafuu na kuondokana na kuuza mazao kabla ya
kukomaa.
·
Wakulima wa mazao ya viungo wamehamasishwa kuanzisha
ushirika wa wakulima, ambapo taratibu za uanzishaji zinaendelea.
5.1.6 Mkakati wa kuongeza kipato cha mwananchi
na pato la Halmashauri ya wilaya kwa mazao mapya
Zao
la Korosho ni miongoni mwa mazao ya
biashara ambayo Wilaya imeanza kuyapa kipaumbele, ambapo kuanzia mwaka 2013/14 mfumo wa stakabadhi ghalani na kuuza
korosho kwa njia ya mnada na kuanzisha mashamba darasa umeanzishwa na
jumla ya hekta 99 zimelimwa. Mwaka 2013/2014 korosho zimeuzwa kati ya
Tshs. 1,250/= na Tshs1,360/= kwa kilo ya
daraja la kwanza na Tshs 900 kwa kilo kwa daraja la pili na jumla tani 4
zimeuzwa kwa utaratibu wa kukusanya na kuuza kwa pamoja bila kutegemea mkopo
toka taasisis za fedha, uvunaji unaendelea, mafanikio machache yameanza
kujitokeza ambapo;
·
Uzalishaji umeongezeka kutoka tani 10 mwaka 2010
/2011 hadi tani 25 mwaka 2012/2013.
·
Miche bora ya korosho 850 imesambazwa na
kupandwa kwa wakulima mwaka 2012/2013. Mashamba darasa 20 yameanzishwa na
kuendelezwa kwa kushirikiana na Bodi ya korosho na madawa ya ruzuku yamesambazwa
kwa wakulima.
·
Elimu ya kilimo bora cha korosho imetolewa kwa
wakulima 300 na wabanguaji 26.
Wilaya
kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho husambaza mbegu na miche bora ya Korosho,
kujengea uwezo Chama cha wakulima wa Korosho Ngomeni
5.1.7 Upatikanaji na matumizi ya zana za kilimo
Wilaya
imeweka juhudi katika kuongeza upatikanaji na matumizi ya zana za kilimo kwa
kuishirikisha sekta binafsi, kuhamasisha na kuwezesha vikundi vya wakulima
katika matumizi ya zana bora za kilimo hususan kwa vijana kupata mikopo ya
pembejeo na zana za kilimo kutoka kwenye mfuko wa pembejeo.
5.1.8 Matumizi ya mbegu bora
Wilaya imefanya juhudi mbalimbali ili kuboresha
uzalishaji wa Mazao. Miongoni mwa juhudi hizo ni pamoja na;
- Uzalishaji wa mbegu za Mahindi zilizothibitishwa (CS – Certified Seeds) ambapo tani 110 zimezalishwa msimu wa 2012/2013
Uzalishaji wa mbegu bora
Mwaka
|
Mahindi ya mbegu
|
Mahindi ya lishe
|
2010
|
Tani 23.9
|
Tani 12
|
2011
|
Tani 64
|
Tani 40
|
2012
|
Tani 1
|
Tani 0
|
2013
|
Tani 60
|
Tani 50
|
- Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) wakulima wa kijiji cha Tongwe wamewawezesha kuwa na kituo chenye mashine ya kusindika muhogo. Kituo hiki kina uwezo wa kuzalisha tani moja kwa wiki.
5.1.9 Mapokezi ya Vocha za Pembejeo za Ruzuku
Wilaya ya Muheza ni miongoni mwa Wilaya
zinazopata pembejeo za ruzuku katika Mkoa wa Tanga. Matumizi ya pembejeo
za Ruzuku yameongezeka toka 34% mwaka 2010/11 hadi 100% mwaka 2012/13 kwa
pembejeo za Ruzuku zilizoletwa hapa Wilayani.
Mgao
wa pembejeo za ruzuku kwa kipindi cha miaka 3 ulikuwa kama ifuatavyo:-
MWAKA
|
2010/2011
|
2011/2012
|
2012/2013
|
2013/2014
|
IDADI YA VOCHA
|
30,000
|
16,800
|
18,000
|
14,400
|
5.1.10 Matumizi ya Trekta
Vikundi 27 pamoja na wamiliki binafsi 13
wa matrekta wamehamasika kutumia matrekta madogo ili kupanua wigo wa eneo la
matumizi ya kilimo na kuongeza uzalishaji. Vikundi na watu binafsi
wamehamasishwa na kuunganishwa na SUMA JKT kwa ajili ya kupata mikopo ya
matrekta, kikundi kimoja na watu binafsi 28 wamejaza fomu wanangoja kufanyiwa
tathmini na SUMA J.K.T. Aidha trekta kubwa moja na power tiller 10 zimenunuliwa
na watu binafsi. Pia Vikundi 25 vyenye wanyama kazi wamepatiwa elimu ya
matumizi bora ya wanyamakazi.
Hadi sasa Wilayani kuna jumla ya matrekta 73 kati
ya hayo matrekta 62 yanafanya kazi na 11 yanahitaji matengenezo.
Matumizi ya matrekta makubwa yameongezeka kutoka 57 mwaka 2010 hadi 73
mwaka 2013
MWAKA
|
2010
|
2011
|
2012
|
2013
|
2014 (hadi Februari)
|
Matrekta makubwa
|
57
|
57
|
70
|
73
|
73
|
Matrekta ya mkono
|
43
|
43
|
45
|
53
|
55
|
JUMLA
|
100
|
100
|
115
|
126
|
128
|
5.1.11 Umwagiliaji
Ibara ya 19 ya ilani ya Chama Chama Tawala
inalenga Kujenga Misingi ya Uchumi wa Kisasa wa taifa linalojitegemea. Ili kuongeza uzalishaji na kuondokana na
kilimo cha kutegemea mvua wananchi wamehamasishwa juu ya kilimo cha umwagiliaji
na uboreshaji wa miundombinu unaendelea ambapo Skimu za umwagiliaji za Misozwe,
Mashewa zinaendelezwa na ya Potwe ipo katika hatua za upembuzi yakinifu ili kubaini maeneo yanayofaa kwa kilimo
cha umwagiliaji. Skimu hizi zitakapokamilika zitakuwa na uwezo wa kumwagilia
hekta 250 (Misozwe 100, Mshewa 50 na Potwe 100). Kupitia Skimu hizo
wilaya inategemea kuongeza uzalishaji wa Mahindi na Mchele kwa tani 2,460. Aidha, Wilaya imenunua pampu rahisi 30 za umwagiliaji na kuzisambaza kwa
vikundi vitatu vya wakulima.
Halmashauri
ya Wilaya imetekeleza jumla ya miradi kumi ya kilimo kwa mwaka 2011/12 hadi
2012/13 yenye thamani ya Ths.1,920,636,494.00.
5.2 SEKTA YA MIFUGO
Ibara ya 38 inasisitiza kuiendeleza Sekta ya
Mifugo kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ili kuiwezesha kutoa mchango
mkubwa kwenye Pato la Taifa. Hapa Wilayani uendelezaji sekta hii unafanywa kwa ushirikiano
na wadau wa mifugo waliopo Wilayani kama vile World visión, Land O’Lakes, Brac
Tanzania na vyama vya ushirika vya msingi na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.
Jumla ya wafugaji 420 wamepatiwa elimu ya
ufugaji wa kibiashara na 320 wamepata mafunzo juu ya matumizi ya majosho yanayozingatia
uhifadhi wa mazingira, pia miundombinu ya mifugo imeboreshwa ikiwemo majosho 2,
mnada1, mabwawa 2 na machinjio 1.
5.2.1 Idadi ya Mifugo na uzalishaji wake
Katika wilaya ya Muheza kuna mifugo
380,854 kati ya hiyo ng’ombe ni 28,747 (chotara 9,915 na asili 18,832), Mbuzi
45,483 (chotara 1,007, asili 44,476), Kondoo 5,457, Nguruwe 2,040, Punda 227 na
kuku wa asili 294,229 na kuku wa mayai 4,671.
5.2.2 Uzalishaji wa maziwa
MWAKA
|
2010/2011
|
2011/2012
|
2012/2013
|
Uzalishaji kwa lita
|
5,525,075
|
6,029,030
|
6,456,550
|
5.2.3 Uzalishaji wa Nyama
MWAKA
|
NG’OMBE (Kg)
|
MBUZI (Kg)
|
KONDOO (Kg)
|
NGURUWE (Kg)
|
2010/2011
|
378,840
|
67,995
|
7,988
|
42,118
|
2011/2012
|
397,100
|
74,190
|
9,945
|
43,001
|
2012/2013
|
399,103
|
76,053
|
10,112
|
43,781
|
1,175,043
|
218,238
|
28,045
|
128,900
|
5.2.4 Uhamilishaji
Huduma ya uhamilishaji inatolewa
kupitia vyama vya ushirika wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa (Muheza – CHAWAMU
na Amani- UWAMA) pamoja na wadau wa sekta binafsi wakiwemo World vision-
Tanzania na Brac Tanzania’ wafugaji hupatiwa huduma hii muhimu kwa njia ya
kukopeshwa na baadaye kulipa wakati wa malipo ya mwezi ya mauzo ya maziwa.
Idadi ya ng’ombe waliohamilishwa na
ndama waliozaliwa katika kipindi cha miaka mitatu ni kama ifuatavyo;
Mwaka
|
Idadi ya ng’ombe
waliopandishwa
|
Idadi ya ndama
|
Idadi ya ndama jike
|
Idadi ya ndama dume
|
2010/11
|
412
|
248
|
123
|
125
|
2011/12
|
439
|
265
|
134
|
131
|
2012/13
|
448
|
269
|
129
|
140
|
Miundombinu sekta ya mifugo imeboreshwa na
jumla ya miradi 7 imetekelezwa yenye thamani ya Shilingi 415,265,267.00 katika kipindi cha
mwaka 2012/2013 hadi Januari, 2014
5.3 USHIRIKA NA MASOKO
Wilaya ina vyama vya ushirika 37 ikiwemo vyama vya
akiba na mikopo 23, Ushirika wa mazao 7 vyenye wanachama 332 na hisa Tsh.
7,224,000/=, vyama vya wafugaji 5 na aina nyingine 2 vyenye wanachama 48 na
hisa zenye thamani ya Tsh. 1,380,000/=
5.3.1 Vyama vya akiba na mikopo (SACCOS)
Mwaka
|
Idadi ya SACCOS
|
Wanachama
|
Hisa
|
Akiba
|
Amana
|
Mikopo (000)
|
||||
Idadi ya vikundi
|
Me
|
Ke
|
Jml
|
Tolewa
|
Rejeshwa
|
|||||
2011
|
22
|
83
|
1448
|
886
|
2417
|
126,794,000
|
785,042,000
|
44,685,000
|
3,360,826
|
1,995,528
|
2012
|
22
|
83
|
1448
|
886
|
2417
|
126,794,000
|
796,080,000
|
46,115,000
|
3,460,826
|
2,095,528
|
2013
|
23
|
105
|
1625
|
840
|
2570
|
130,561,000
|
805,262,000
|
62,142,000
|
3,673,493
|
2,624,524
|
5.3.2 Vyama vya wafugaji
Mwaka
|
Idadi
|
Wanachama
|
Hisa
|
||
Me
|
Ke
|
Jml
|
|||
2011
|
3
|
737
|
269
|
1006
|
9,810,000
|
2012
|
3
|
737
|
269
|
1006
|
9,810,000
|
2013
|
5
|
833
|
327
|
1160
|
13,605,000
|
5.4 SEKTA YA UVUVI
Uvuvi hapa Wilayani unafanyika katika bahari ya Hindi
hasa kwa wakazi wa kata ya Kigombe na kwenye mabwawa ya ufugaji samaki. Kuna
mabwawa 6 yaliypandikiwa samaki aina ya sato kwa ajili ya kuzalisha vifaranga
katika Kata ya Misozwe.
Ili kuboresha shughuli za uvuvi Wilayani
kwa kipindi cha Januari - Desemba 2012/13 wavuvi na wachuuzi 120 wamepatiwa
mafunzo juu ya udhibiti wa ubora wa mazao ya uvuvi ili kukidhi mahitaji ya soko
la ndani na nje katika Kata ya Kigombe. Aidha Wilaya imefanya doria shirikishi
12 kati ya hizo doria za baharini 9 na nchi kavu 3 dhidi ya uvuvi haramu.
Aidha
Wilaya imetekeleza jumla ya miradi nane ya Sekta ya Mifugo kwa mwaka 2011/12
hadi 2012/13 yenye thamani ya Ths.
448,390,522.00.
5.5 SEKTA YA BARABARA, MAWASILIANO NA UCHUKUZI
Njia kuu ya usafiri
zinazotumiwa na Wananchi Wilayani ni
barabara. Aidha mawasiliano ya simu za mkononi yanapatikana, Mitandao
inayopatikana Wilayani Muheza ni Tigo, Airtel,
Vodacom na Zantel. Mitandao ya simu imerahisisha huduma za mawasiliano Vijijini
na huduma za fedha. Aidha imesaidia kuboresha biashara na masoko ya bidhaa ya
mazao ya Kilimo kwani simu zinatumika kuwaunganisha wateja na wakulima.
5.5.1 Barabara
Mtandao wa barabara
Wilayani una urefu wa kilometa 818.2 kati
ya hizi kilometa 693 zinasimamiwa na Wilaya na kilometa 125.2 zinasimamiwa na wakala wa barabara Tanzania yaani TANROADS. Kati
ya kilomita 818.2 barabara kuu ni km 42, barabara za mkoa km 83.2, barabara za
Wilaya /Vijiji km 673.4 na kilomita 19.6 barabara za Mjini.
Mtandao wa
barabara zinazopitika kwa kipindi cha mwaka mzima umeongezeka toka kilomita 250
mwaka 2010/11 hadi 393 mwaka 2012/13 kama inavyoonekana kwenye jedwali.
MWAKA
|
2010/2011
|
2011/2012
|
2012/2013
|
Barabara zinazopitika kwa mwaka mzima.
|
250
|
309
|
393
|
Aidha vijiji 2 havijaunganishwa na mtandao
wa barabara, Pia baadhi ya barabara zinapitika kwa shida kipindi cha msimu wa
mvua ikiwemo barabara za Zigi - Kwemdimu, Lunguza - Kambai na Potwe - Kimbo. Wananchi
hupata usumbufu wa kufikisha bidhaa zao
sokoni kutokana na hali ya barabara. Wilaya inaendelea kutekeleza matengenezo ya barabara
mbalimbali Wilayani ili kuboresha usafiri na mawasiliano.
Halmashuri ya Wilaya hutumia wastani wa Tsh.
750,000,000/= kwa mwaka katika matengenezo ya barabara, ambazo zimesaidia
kuimarika kwa barabara za Wilaya.
Aidha Wilaya
imetekeleza jumla ya miradi hamsini na tatu kwa mwaka 2011/12 hadi 2012/13 yenye thamani ya Ths. 968,934,500.00.
5.6 SEKTA ARDHI, MALIASILI NA
MAZINGIRA
5.6.1 Sekta ya Ardhi
Wilaya ya Muheza ina jumla ya
kilomita za mraba 1974 ambapo zinajumuisha ukanda wa bahari. Eneo linalofaa kwa
kilimo ni 85% ya eneo la Wilaya. Hata hivyo sehemu kubwa ya eneo hilo ni sehemu
ya mashamba makubwa ya mkonge, mpira na mifugo ambayo yanamilikiwa na
watu/mashirika na ambayo hayaendelezwi ipasavyo yenye eneo la hekta 59,795.32.
Hii inapelekea kuwepo kwa migogogo mingi ya ardhi. Migogoro hiyo ya ardhi
inahusu uvamizi katika mashamba makubwa yaliyotelekezwa.
Pamoja na migogoro ya mashamba pia
ipo migogoro ya mipaka ya Wilaya, mgogoro kati ya Serikali na Wananchi, migogoro
ya mipaka ya vijiji na migogoro ya viwanja. Maeneo yenye migogoro ni pamoja na
mashamba 7 ya Mkonge, shamba la mifugo lililopo Azimio na shamba la mifugo la
Mivumoni.
Aidha kuna mgogoro wa mpaka kati ya
Wilaya ya Muheza na Wilaya za Tanga na Pangani. Hatua za kutatua mgogoro uliopo
kati ya Wilaya ya Tanga na Muheza unaendelea kushughulikiwa katika ngazi ya
Mkoa na ule kati ya Wilaya ya Muheza na Pangani mazungumzo kati ya uongozi wa
Wilaya hizo mbili bado yanaendelea ili kufikia muafaka.
5.6.2 Ufumbuzi wa migogoro ya mashamba
Halmashauri ya
Wilaya imefanya taratibu za kuomba kubatilishwa kwa miliki za Mashamba yaliyotelekezwa
yenye ukubwa wa eneo la hekta 24,627 kwa kufanya mambo yafuatayo:-
·
Kuwasilisha mapendekezo kwenye Baraza la
Halmashauri ambalo lilidhiinisha mapendekezo ya kufutwa kwa hatimiliki za
Mashamba hayo ili wagawiwe wananchi wenye uhaba wa Ardhi ya kilimo
·
Uamuzi wa baraza la Madiwani uliwasilishwa kwa
kamishna wa Ardhi kwa barua kumb. Na MUD/ASF/VOL/IV /35 ya tarehe 21/9/2007.
·
Wilaya iliendelea kufanya mawasiliano ya muda
mrefu na ilipofika mwaka 2009, Wizara ya Ardhi iliielekeza taratibu za kisheria
zifuatwe kwa kutuma notisi kwa wamiliki wa Mashamba. Utekelezaji ni kama inavyo
onekana kwenye jedwali hapa chini.
Na
|
Jina la shamba
|
Mmilikli
|
Tarehe ya kutuma notisi
|
Tarehe ya majibu
|
Tarehe ya kutuma mapendekezo wizara ya
ardhi
|
Ukubwa Hekta
|
|
1.
|
KIBARANGA
|
Consolidated
holding corporation
|
2/6/2009
|
6/8/2009
|
6/10/2009
|
5,647
|
|
2.
|
SAGULAS
|
Consolidated
holding corporation
|
2/6/2009
|
|
17/11/2009
|
500
|
|
3
|
LEWA
|
Consolidated
holding corporation
|
2/6/2009
|
|
17/11/2009
|
3,901
|
|
4
|
GEIGLTZ(Azimio
kilapula)
|
Consolidated
holding corporation
|
2/6/2009
|
6/8/2009
|
17/11/2009
|
4,902
|
|
5
|
KIHUHWI
|
Consolidated
holding corporation
|
2/6/2009
|
6/8/2009
|
17/11/2009
|
602
|
|
6
|
SONGA
|
Jeshi la
wananchi
|
2/9/2009
|
14/7/2009
|
17/11/2009
|
1,000
|
|
7
|
KWAFUNGO
|
G. Chavda (Tan
farms
|
163/2010
|
Haikujibiwa
|
7/5/2009
|
2,345
|
|
8
|
BWEMBWERA
|
AMC limited
Arusha
|
2/2/2010
|
Imerudishwa
|
7/5/2010
|
5730
|
|
JUMLA
|
24,627
|
·
Consolidated holdings walijibu notisi ya
Halmashauri kwa barua kumb. Na.
CHC/DV/1/13/288 YA tarehe 2/0/2009 wakiiomba Halmashauri isitishe zoezi la
ubatilishaji kwa malezo kwamba wanatarajia kuyapima upya mashamba hayo na kwamba
baada ya kupimwa watawapatia wawezekaji binafsi pamoja na wakulima wadogo
wadogo. Halmashauri haikukubaliana na suala hilo kwani sehemu kubwa ya mashamba
hayo imekwishavamiwa na kupandwa mazao ya kudumu na kuendelezwa kwa makazi.
·
Tarehe 2/10/2009 Halmashauri ya Wilaya
ilimuandikia Kamishina wa Ardhi barua yenye kumb. Na. MUDF /44/121 kumuomba
aendelee na taratibu za ufutaji wa miliki.
·
Taratibu za ufutaji zinaendelea na kwa mara ya
mwisho wizara ya Ardhi iliomba kutumiwa upya baadhi ya nyaraka za mapendekezo
ya ubatilishaji wa miliki za mashamba yaliyopelekewa notisi. Nyaraka zimetumwa
upya kwa Kamishina wa Ardhi kwa barua kumb. Na. MUDF/44/127 ya tarehe
16/2/2012.
·
Aidha nyaraka nyingine mpya zilitumwa kwa
Kamishina wa Ardhi kwa barua kumb. Na. HW/MUH/A.10/2VOL.III/5 ya tarehe 19/10/2012.
·
Kwasasa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
inaendelea kufuatilia kwa kuwasiliana na Wizara ya ardhi.
Pamoja na kuomba kubatilisha hati
miliki za ardhi kwa baadhi ya mashamba, Wilaya inaendelea kushughulikia
migogoro mingine kwa kufuata taratibu nyingine.
Baadhi ya migogoro imekwisha hususani mgogoro
wa shamba mkonge Zeneth, mgogoro kati ya Kijiji cha Kibaoni na Mlingano na
Mgogoro wa Kijiji cha Kiwanda na Kwafungo. Kesi zingine bado zipo mahakamani,
kama ifuatvyo ;
·
Migogoro
ya viwanja 148 imetatuliwa kati ya migogoro 150
·
Mgogoro
wa shamba 1 umetatuliwa kati ya Migogoro 14 (13 usuruhishi unaendelea).
5.6 3 Hati miliki za ardhi.
Mashamba na viwanja 844 vimepatiwa
hati
Umiliki
|
2011
|
2012
|
2013
|
Hati miliki za
viwanja/mashamba
|
486
|
832
|
844
|
Upimaji wa viwanja
|
3,232
|
3,577
|
3,582
|
Jumla ya Michoro 3 imeandaliwa
katika maeneo ya shamba la Chatur ikiwa na viwanja 330, Kwemkabala Viwanja 317
na Sega viwanja 22. Hati miliki zitatolewa mara baada ya taratibu za ugawaji
kukamilika.
5.7 SEKTA YA MALIASILI NA MISITU
5.7.1 Misitu
Wilaya ina jumla ya hekta 47,000 za misitu, kati
yake ni msitu wa asili wa Amani (ANR) uliopo katika Tarafa ya Amani. Msitu huu
una viumbe mbalimbali adimu duniani pamoja na uoto wa asili unaovutia wanyama
kuishi. Wanyama wanaopatikana katika
Msitu huu ni pamoja na Kima weupe, Nyoka, Vinyonga, tumbili na wengineo wengi. Pia
Wilaya inayo misitu mingine ya asili 9 (Kwemarimba, Mlinga, Manga, Kambai,
Nilo, kwani, Tongwe, Lunguza na Derema). Wilaya inaendeleza jitihada za kuhifadhi,
kulinda, kuendeleza, uboreshaji na kuvuna maliasili za misitu na Nyuki kwa
manufaa ya Taifa kama inavyoelekezwa katika ibara ya 44 ya Ilani ya Chama
Tawala.
5.7.2 Ufugaji wa nyuki
Shughuli za ufugaji nyuki zinafanyika
katika vijiji 8 ndani ya Tarafa 2 hapa Wilayani. Uzalishaji wa mazao ya nyuki umekuwa
ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka tani 2,400 za asali na 150 za nta hadi tani
4000 za asali na 200 za nta. Msisitizo
umewekwa katika matumizi ya zana bora za ufugaji nyuki ambapo jumla ya mizinga
140 imegawiwa kwa wafugaji, na mingine 100 imenunuliwa tayari kwa kugawiwa.
Hali ya uzalishaji asali na nta ni
kama inavyoneshwa hapa chini :-
Uzalishaji mazao ya nyuki
Mwaka
|
Idadi ya Mizinga
|
Uzalishaji (kg)
|
|
Asali
|
Nta
|
||
2010/2011
|
300
|
2400
|
150
|
2011/2012
|
350
|
2900
|
170
|
2012/2013
|
500
|
4000
|
200
|
2013/2014
|
1473
|
4500 (Matarajio)
|
300 (matarajio)
|
5.7.3 Utunzaji Mazingira.
Vijiji 15 vimeanzisha hifadhi ya
misitu ya asili ambapo shughuli za utunzaji wa mazingira hufanyika. Kampeni za
upandaji miti na uthibiti wa moto zinafanyika kila mwaka na hali ya upandaji
miti ni kama inavyoonekana katika jedwali ;
MWAKA
|
IDADI YA MITI ILIYOPANDWA
|
2010
|
4,800,000
|
2011
|
2,250,300
|
2012
|
2,300,120
|
2013
|
1,516,198
|
Doria za mara kwa mara zinafanyika
katika maeneo ya misitu na ukanda wa bahari. Pia Wilaya imewaondoa wavamizi
waliovamia misitu ya Kwani na Tongwe na jumla ya miti 1,516,198 ya matunda,
kuni, kivuli, mbao na viungo imepandwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali
hususani shule, mashirika na watu binafsi kwa ajili ya kuendeleza hifadhi ya
mazingira.
Kampeni dhidi ya athari za moto
imefanyika katika vijiji 32 vilivyo karibu na misitu ili kunusuru bionuai.
Wananchi wanaoishi karibu na misitu ya hifadhi wamehamasishwa kufanya shughuli
za ufugaji nyuki na vipepeo kwani shughuli hizi ni rafiki kwa Mazingira. Pia
elimu inaendelea kutolewa juu ya
umuhimu wa misitu na athari za uharibifu wa mazingira.
5.8 SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO
5.8.1 SEKTA YA VIWANDA
Wilaya ina jumla
ya biashara ndogo na za kati 3030, kati ya hizo viwanda vidogo ni 11, Jumla ya
ajira zitolewazo na sekta ya Viwanda, Biashara na masoko ni 4,963 ambayo ni
sawa na 2.1%. Wilaya inafanya juhudi za kukuza sekta ya viwanda, biashara na
masoko kutoka 2.1% ya sasa hadi 3% ifikapo mwaka 2015 kwa kuboresha mazingira
ya uwekezaji, kujenga masoko 2 mapya na kukarabati 1 ili kuweka mazingira
mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta za viwanda,biashara na masoko.Hivyo
kukuza pato la mtu binafsi, Halmashauri na Taifa.
5.8.2 JUKWAA LA UWEKEZAJI
Wilaya imeshiriki katika jukwaa la uwekezaji la
Kanda ya Kaskazini lililofanyika Mkoani Tanga, ambapo Fursa za uwekezaji
zilizopo Wilayani zilitangazwa. Wawekezaji kumi na mmoja wameonyesha nia
ya kuwekeza katika sekta za kilimo, kuongeza thamani mazao ya viungo na
matunda, ujenzi wa makazi na hoteli na utalii wa kiikolojia.
Wawekezaji 2 wenye nia ya
kuwekeza katika kuongeza thamini ya matunda na kusindika mihogo taratibu za
kuwapatia ardhi zinaendelea, na wengine wenye nia ya kuwekeza katika kilimo na
ujenzi wa makazi na hoteli mazungumzo yanaendelea.
6.0 SEKTA ZA HUDUMA ZA JAMII
6.1 SEKTA YA MAJI
6.1.1 Hali ya upatikanaji wa
maji Muheza Vijijini
Watu wapatao 110,679 sawa na 62.2% ya wakazi wanaoishi Vijijini wanapata Maji safi kutokana
na vyanzo mbalimbali kama ifuatavyo:-
Miradi ya maji ya bomba ya mtiririko10,
Miradi ya maji ya bomba ya kusukumwa na mashine 7, Visima vifupi vyenye pampu
za mikono 175, Visima virefu vyenye pampu za mikono 23.
Hali ya upatikanaji wa maji vijijini
Mwaka
|
2010
|
2011
|
2012
|
2013
|
Hali ya upatikanaji wa maji
|
55.4%
|
56.3%
|
56.3%
|
62.2%
|
Jumla ya miradi 4 ya maji mteremko (Gravity
schemes) yenye thamani ya Ths. 839,642,117.00 imekamilika kupitia mradi wa Maji
na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) ambapo jumla ya watu 3,649 wamenufaika
na miradi hiyo, miradi 3 ambayo inakadiriwa kugharimu Tsh. 724,722,350.00
utekelezaji unaendelea na jumla ya watu 3,762 watanufaika na miradi hii ifikapo
mwishoni mwa mwaka 2013/14.
6.1.2 Huduma ya maji Muheza Mjini
Mji wa Muheza una jumla ya wakazi 30,834 kutokana
na sensa ya Taifa ya watu na makazi ya Mwaka 2012, kati yao watu 3916 sawa na
asilimia 12.7% ndio wanaopata maji safi.
Huduma ya Maji ya Bomba inayotolewa Muheza Mjini
inatoka katika chanzo cha Maji cha Mto Mkulumuzi unaoanzia kwenye milima ya
Magoroto. Kiasi cha maji kinachozalishwa
katika chanzo hiki wakati wa mvua ni wastani wa Mita za ujazo 1,425 kwa siku na
mahitaji ya wakazi wa Muheza Mjini ni Mita za ujazo 4,831 kwa siku. Mradi wa
Maji ya bomba Muheza Mjini umeshapitwa na wakati kwani ulijengwa Mwaka 1977 kwa
kukidhi idadi ya watu wapatao 8,000.
Hali ya upatikanaji wa maji Mjini kwa asilimia
Mwaka
|
2010
|
2011
|
2012
|
2013
|
Hali ya upatikanaji wa maji
|
17
|
25
|
20.5
|
12.7
|
6.1.3 Mkakati wa kupunguza tatizo la
Maji Muheza Mjini.
Wilaya imechukua jitihada mbali mbali ili
kukabiliana na tatizo la maji Muheza mjini. Miongoni mwa jitihada hizo ni
pamoja na;
·
Kuchimba
kisima cha Polisi Mang’enya kinachotumia umeme jua na chenye uwezo wa kutoa
lita 5,000.
·
Kuendeleza
kisima cha kitisa kilichokuwa kinatumiwa na Mamlaka ya mkonge ambapo gharama ya
mradi ilimekadiriwa kuwa kiasi cha Tsh.806 milioni, kiasi cha Tsh. 229
zilitengwa toka mapato ya ndani na kuanza utekelezaji wa Mradi huu.
·
Visima
virefu 9 vimechimbwa na vimefanyiwa upimaji wa ubora na wingi wa maji.
·
Wilaya
iko kwenye mchakato wa kununua mtambo wa kuchimbia Visima kwa gharama ya Tshs 250,000,000/=
6.1.4 Uvunaji wa maji ya mvua
Wilaya kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo wakiwemo World Vision,
World Bank na wengineo imejengakwishajenga miundombinu ya uvunaji wa maji ya
mvua katika shule za msingi 11,
Sekondari 5 na Zahanati 8. Aidha jumla ya miradi 6 ya programu ya maji vijijini
inayoendelea kujengwa ina kipengele cha ujenzi wa miundombinu ya maji katika
taasisi za kijamii.
Ili kuongeza upatikanaji wa maji Mjini na
Vijijini, Wilaya inaendelea kufanya uhamasishaji wa ujenzi wa miundombinu ya
uvuanaji kwa kila nyumba iliyojengwa kwa bati.
Aidha
Wilaya imetekeleza jumla ya miradi kumi na mmoja kwa mwaka 2011/12 hadi 2012/13 yenye
thamani ya Ths. 2,416,503,740.00.
6.2 SEKTA YA ELIMU
Elimu ya Msingi
Wilaya ya Muheza ina
jukumu la kusimamia huduma za elimu kwa wananchi wake. Huduma ya sekta ya Elimu
inajumuisha usimamizi na utoaji huduma katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya
Msingi, Elimu ya watu wazima, mafunzo ya ufundi stadi, elimu maalum, utamaduni
na michezo.
6.2.1 Elimu ya Awali
Wilaya ya Muheza ina
jumla ya madarasa ya elimu ya awali 113 kati ya hayo madarasa 109 yapo katika
shule za msingi za Serikali na madarasa 4 yapo katika shule zinazosimamiwa na
mashirika yasiyo ya Kiserikali. Idadi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hizo
ni kama ifuatavyo:
MWAKA
|
IDADI YA SHULE ZA AWALI
|
IDADI YA WANAFUNZI WA AWALI
MWAKA 2011 – 2013
|
|||||||
SHULE ZA SERIKALI
|
SHULE ZISIZO ZA SERIKALI
|
||||||||
SERIKALI
|
BINAFSI
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
|
2011
|
108
|
3
|
111
|
2887
|
2890
|
5777
|
196
|
217
|
413
|
2012
|
108
|
4
|
112
|
3122
|
3053
|
6175
|
251
|
241
|
492
|
2013
|
109
|
4
|
113
|
3255
|
3186
|
6441
|
194
|
168
|
362
|
Hali ya
mahudhurio ya wanafunzi wa awali ni 90% . Elimu hii kwa kiwango kikubwa
hufanikishwa kwa kutegemea miundo na walimu wa shule za msingi
6.2.2 ELIMU YA MSINGI
Wilaya ina jumla ya shule za
msingi 115 kati ya hizo shule 111 ni za Serikali na shule 4 ni za mashirika
yasiyo ya Kiserikali. Aidha shule 109 za Serikali zina darasa la I-VII na shule
2 hazijafika darasa la VII. Idadi ya wanafunzi darasa la I – VII kwa shule za
Serikali ni 37,654 na shule za mashirika yasiyo ya Kiserikali ni 1,110. Jumla
ya wanafunzi 7,287 wameandikishwa darasa la kwanza katika shule za Serikali na
wanafunzi 251 wameandikishwa katika shule zisizo za Serikali.
Jedwali lifuatalo linaonesha mchanganuo wa
uandikishaji kwa Mwaka 2011 – 2013
MWAKA
|
UANDIKISHWAJI DARASA LA 1
|
IDADI YA WANAFUNZI DARASA LA I – VII
|
|||||
WAV
|
WAS
|
JUMLA
|
%
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
|
2011
|
4,010
|
3,628
|
7,638
|
100
|
20,517
|
20,043
|
40,560
|
2012
|
3,771
|
3,656
|
7,427
|
100
|
19,672
|
19,650
|
39,322
|
2013
|
3,865
|
3,673
|
7,538
|
100
|
18,790
|
18,864
|
37,654
|
6.2.2.1 Hali ya upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia
Hadi kufikia mwezi
Desemba mwaka 2013 uwiano wa kitabu kwa
mwanafunzi ni 1:3 kutoka 1:7 mwaka 2011 na 2012. Haya ni mafanikio makubwa
yaliyotokana na ongezeko la vitabu kutokana na fedha za capitation na vitabu
kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Aidha Wilaya imenunua vitabu 5,396 kwa fedha za capitation
mwaka 2012/2013 na hadi kufikia Desemba
2013 Wilaya imepokea na
kusambaza vitabu 105,000 katika shule zote 111 toka wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na fedha za rada, hivyo kufanya jumla ya vitabu 110,396
vilivyopelekwa mashuleni hadi Desemba 2013.
6.2.2.2 Hali ya walimu
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina jumla ya walimu wapatao 888. Idadi ya
walimu haitoshelezi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu, kufariki na
kujiendeleza.
Mahitaji ya Walimu 2011 – 2013
MWAKA
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
ASILIMIA (%)
|
2011
|
1014
|
1001
|
13
|
1.3
|
2012
|
984
|
971
|
13
|
1.3
|
2013
|
981
|
888
|
93
|
9.5
|
6.2.2.3 Hali ya miundombinu.
AINA
|
MAHITAJI
|
YALIYOPO
|
UPUNGUFU
|
Madawati
|
13,589
|
12,074
|
1,515
|
Nyumba za walimu
|
1,161
|
133
|
1,060
|
Madarasa
|
1,055
|
635
|
420
|
Viti
|
2,431
|
1,238
|
1,193
|
Meza
|
2,346
|
1,116
|
1,230
|
Vyoo
|
1,843
|
1,029
|
814
|
TRcs
|
29
|
4
|
25
|
6.2.2.4 Ufaulu
Mafanikio katika
jitihada za kuboresha Elimu ya msingi wilayani yanajidhihirisha kwa kuangalia
matokeo ya mtihani wa darasa la IV na VII mwaka 2011 – 2013.
Matokeo ya Darasa la saba kwa kigezo cha alama
100: 2011 – 2013
Mwaka
|
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Waliochaguliwa
|
|||||||||
Wav
|
Was
|
Jml
|
Wav
|
Was
|
Jml
|
%
|
Wav
|
Was
|
Jml
|
%
|
Nafasi
kimkoa
|
|
2011
|
2667
|
2717
|
5384
|
1789
|
1785
|
3574
|
66
|
1789
|
1785
|
3574
|
100
|
6
|
2012
|
2028
|
2341
|
4369
|
552
|
639
|
1191
|
27
|
1391
|
1681
|
3077
|
258
|
7
|
2013
|
2031
|
2181
|
4212
|
1311
|
1467
|
2778
|
66
|
1311
|
1467
|
2778
|
100
|
4
|
Matokeo Darasa la IV: 2011 – 2013
Mwaka
|
Waliofanya Mtihani
|
Waliofaulu Mtihani
|
|||||
Wav
|
Was
|
Jml
|
Wav
|
Was
|
Jml
|
%
|
|
2011
|
2508
|
2544
|
5052
|
2362
|
2446
|
4808
|
95
|
2012
|
2447
|
2523
|
4970
|
2191
|
2270
|
4461
|
90
|
2013
|
2379
|
2563
|
4942
|
2300
|
2523
|
4822
|
96
|
6.2.2.5 Matarajio ya baadae
Kuongeza
asilimia ya ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la IV kutoka asilimia 96% mwaka 2013
hadi 100% ifikapo mwaka 2014 na wanafunzi wa darasa la saba kwa kigezo cha
alama 100 kutoka 66% mwaka 2013 hadi kufikia 70% 2014.
6.2.2.6 Hali ya utoro 2011 – 2013
Hali ya utoro mashuleni imepungua kwa kiasi cha
asilimia 72% kutokana na juhudi zilizofanywa na Uongozi wa Wilaya.
Miongoni mwa juhudi hizo ni kuwaelimisha
wazazi/walezi umuhimu wa kuwaandikisha watoto shule za jirani na makazi
wanakotoka ili kupunguza umbali, kuanzisha chakula shuleni, kushirikiana na
kamati za shule pamoja na kutoa elimu juu ya athari za utoro. Jedwali kuonesha
hali ya utoro 2011 – 2013.
Mwaka
|
Wav
|
Was
|
Jml
|
2011
|
82
|
54
|
136
|
2012
|
63
|
52
|
115
|
2013
|
55
|
45
|
100
|
6.2.2.7 Elimu Maalumu
Wilaya ina kituo kimoja cha ulemavu wa akili katika
Shule ya Msingi Masuguru chenye wanafunzi 38 kati yao Wav 24 na Was 14. Vile
vile Wilaya imeanzisha kitengo cha wanafunzi
viziwi mwanzoni mwa Januari 2014 katika Shule ya Msingi Mbaramo. Hata hivyo mkakati
wa mwaka 2014 ni kuendelea na kuimarisha utoaji wa Elimu Jumuishi ambapo
wanafunzi wenye ulemavu wataandikishwa katika shule za kawaida za msingi
wilayani.
6.2.2.8 Elimu ya watu wazima
Wilaya ina vituo vya MUKEJA
vinavyoendeshwa katika maeneo mbalimbali hapa Wilayani.
Wilaya imeboresha miundombinu ikiwemo
madarasa, vyoo, madawati na nyumba za walimu kwa kutekeleza miradi 11 yenye
thamani ya Tsh. 149,000,000 katika mwaka wa fedha 2012/2013 hadi Januari, 2013.
Aidha Wilaya imetekeleza jumla ya
miradi mitano kwa mwaka 2011/12 hadi 2012/13
yenye thamani ya Ths. 109,363,636.00.
6.2.3 ELIMU YA SEKONDARI
Wilaya ina shule za Sekondari 30, kati ya hizo 5 zinamilikiwa na watu binafsi
pamoja na mashirika ya dini.
Idadi ya wanafunzi waliopo shule za Serikali kwa
mwaka 2013 ni 9,099 kati yao wavulana
4,451 na wasichana ni 4,648 wakati wanafunzi waliopo shule za Binafsi ni 1,576
wavulana ni 900 na wasichana 676. Hivyo jumla ya wanafunzi wote waliopo shule
za Sekondari kwa mwaka 2013 kuwa 10,675. Aidha wanafunzi wanaotarajia kujiunga
na masomo ya kidato cha kwanza kwa shule za kutwa kwa mwaka 2014 ni 2763 kati
yao wavulana ni 1302 wasichana ni 1461
6.2.3.2 Usajili wa Wanafunzi Kidato cha Kwanza
Usajili kidato cha I
Mwaka
|
Waliochaguliwa
|
Walioripoti
|
Wasioripoti
|
2011
|
3574
|
3133
|
441
|
2012
|
3077
|
2232
|
845
|
2013
|
2778
|
2621
|
157
|
2014
|
2807
|
1472
|
1335 (hadi Januari 31)
|
Wanafunzi 170
sawa na asilimia 5.46% kwa mwaka 2012 wamejiunga na shule binafsi ndani na nje
ya wilaya ya Muheza na wengine kubadilishiwa shule nje ya wilaya ya Muheza.
Asilimia 6.36%
ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha Kwanza sawa na wanafunzi 198
hawakuripoti shuleni kwa sababu mbalimbali pamoja na jitihadi za kuwatafuta
kutofanikiwa. Kwa mwaka 2014 bado usajili unaendelea hadi itapofika mwezi
Machi.
6.2.3.2 Hali ya walimu
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina jumla ya walimu wa Sekondari wenye
shahada na stashahada za ualimu wapatao
431 walioko vituoni. Idadi ya walimu
inatosheleza kwa masomo ya sanaa na lugha. Aidha wilaya inahitaji walimu
144 wa Sayansi na Hisabati, waliopo ni 69 na upungufu ni 75.
Ikama ya walimu
Mwaka
|
Sayansi
|
Sanaa
|
Walimu wote
|
||||||
Mahitaji
|
Waliopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Waliopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Waliopo
|
Upungufu
|
|
2011
|
100
|
59
|
41
|
300
|
216
|
-74
|
400
|
275
|
125
|
2012
|
100
|
64
|
36
|
300
|
309
|
+9
|
400
|
373
|
127
|
2013
|
144
|
69
|
75
|
300
|
362
|
+62
|
444
|
431
|
13
|
6.2.3.3 Hali ya miundombinu.
Aina
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Madawati
|
9,099
|
9146
|
47 ziada
|
Nyumba za walimu
|
365
|
37
|
328
|
Madarasa
|
375
|
268
|
107
|
Vyoo
|
564
|
220
|
344
|
6.2.3.4 Hali ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia
Hadi kufikia
Desemba 2013 uwiano wa kitabu kwa mwafunzi ni 1:3 hii ni mafanikio makubwa
ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo uwiano ulikuwa 1:8.
6.2.3.5 Hali ya Utoro
Hali ya utoro shuleni imepungua kwa asilimia 70%
ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo wanafunzi wengi walikuwa hawamalizi
kidato cha nne kwa sababu ya utoro pia wazazi wengi wameelewa umuhimu wa shule
na watoto wengi wanasoma shule za jirani.
Aidha kati ya sababu kuu zinazopelekea utoro ni mimba ambapo kwa mwaka
2011 waliopata ujauzito walikuwa 57, 2012 walikuwa 33 na 2013 walikuwa 29.
6.2.3.6 Maabara za Sayansi.
Hadi sasa Halmashauri
ya wilaya ina maabara 8 kwa masomo ya sayansi kati ya 75 zinazohitajika, meza za
maabara (mobile laboratory) 7 na madarasa ya
sayansi 17 (Vyumba vya sayansi) kwa shule za Serikali, ujenzi wa maabara
67 katika shule zote za serikali upo katika hatua mbalimbali kwa kutumia fedha za Serikali na nguvu za
Wananchi.
·
7 hatua umaliziaji.
·
2 hatua ya Lenta.
·
5 Ujenzi wa Boma
·
8 hatua ya kumwaga jamvi.
·
16 msingi umekamilika
·
20 hatua ujenzi wa msingi
·
5 Maandalizi ya awali
·
6 utekelezaji haujaanza
Lengo ni kuhakikisha kuwa Shule zote za Serikali zinakuwa na maabara tatu
kwa masomo ya sayansi hadi Novemba mwaka 2014.Wilaya imejipanga kukamilisha
ujenzi huo ambapo mikakati mbalimbali imewekwa ikiwemo:-
·
Michango ya wananchi kwa kila Kijiji
·
Michango ya Watumishi kuchangia kwa ngazi za
mishahara
·
Mfuko wa Jimbo shule 16 zimepata Mgao wa bati 100
kila shule
6.2.3.7 Matokeo ya mitihani ya kidato cha Pili, Nne na Sita
A: KIDATO CHA PILI KUANZIA MWAKA 2010
HADI 2013
|
|||||||||||||||||||
MWAKA
|
WALIOFANYA
|
MADARAJA YA UFAULU
|
% YA UFAULU
|
||||||||||||||||
A
|
B
|
C
|
D
|
F
|
|||||||||||||||
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
||
2010
|
1400
|
1389
|
2789
|
0
|
0
|
0
|
16
|
6
|
22
|
167
|
57
|
224
|
254
|
191
|
445
|
976
|
1125
|
2101
|
25
|
2011
|
1209
|
1140
|
2349
|
0
|
0
|
0
|
7
|
2
|
9
|
105
|
48
|
153
|
276
|
175
|
451
|
787
|
981
|
1768
|
26
|
2012
|
967
|
987
|
1954
|
0
|
0
|
0
|
4
|
9
|
13
|
114
|
54
|
168
|
230
|
211
|
441
|
629
|
721
|
1350
|
32
|
2013
|
923
|
1231
|
2154
|
2
|
2
|
4
|
39
|
5
|
44
|
215
|
184
|
399
|
247
|
356
|
603
|
416
|
672
|
1088
|
49
|
Jumla ya
watahiniwa 2,557 walifanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne kati yao
wanafunzi 474 walifaulu daraja la kwanza hadi la nne sawa na 18.53% mwaka 2012
na mwaka 2013 ni wanafunzi 775 kati ya 2138 (36.2%) ya waliofanya mtihani.
B: KIDATO CHA NNE KUANZIA
MWAKA 2010 HADI 2013
|
|||||||||||||||||||
MWAKA
|
WALIOFANYA
|
MADARAJA YA UFAULU
|
% YA UFA
ULU
|
||||||||||||||||
DIV - I
|
DIV II
|
DIV III
|
DIV IV
|
FAILED
|
|||||||||||||||
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
||
2010
|
941
|
896
|
1837
|
1
|
0
|
1
|
11
|
1
|
12
|
34
|
2
|
36
|
299
|
176
|
475
|
636
|
756
|
1392
|
29
|
2011
|
1057
|
1029
|
2086
|
1
|
0
|
1
|
3
|
0
|
3
|
22
|
5
|
27
|
281
|
156
|
429
|
738
|
851
|
1589
|
22
|
2012
|
1298
|
1258
|
2556
|
1
|
0
|
1
|
8
|
2
|
10
|
37
|
13
|
50
|
274
|
146
|
420
|
819
|
936
|
1745
|
19
|
2013
|
1102
|
1029
|
2138
|
8
|
1
|
9
|
32
|
17
|
49
|
119
|
54
|
173
|
301
|
244
|
544
|
35
|
713
|
1064
|
36
|
Wanafunzi 56 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano sawa na
11.81% ya wanafunzi waliofaulu Mtihani kwa mwaka 2013.
Aidha wanafunzi 129 walifanya mtihani wa kumaliza kidato cha sita kati
yao wanafunzi 111 sawa na 86% walipata daraja la kwanza hadi la nne na
wanafunzi 85 wanatarajiwa kujiunga na Vyuo Vikuu .
C: KIDATO CHA SITA KUANZIA
MWAKA 2010 HADI 2013
|
|||||||||||||||||||
MWAKA
|
WALIOFANYA
|
MADARAJA YA UFAULU
|
% YA UFAULU
|
||||||||||||||||
DIV - I
|
DIV II
|
DIV III
|
DIV IV
|
FAILED
|
|||||||||||||||
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
||
2010
|
30
|
12
|
42
|
0
|
0
|
0
|
0
|
1
|
1
|
9
|
6
|
15
|
13
|
3
|
16
|
8
|
2
|
10
|
76
|
2011
|
37
|
39
|
76
|
1
|
0
|
1
|
7
|
2
|
9
|
20
|
20
|
40
|
6
|
12
|
18
|
6
|
2
|
8
|
89
|
2012
|
46
|
48
|
94
|
0
|
0
|
0
|
5
|
0
|
5
|
20
|
15
|
35
|
13
|
19
|
32
|
8
|
14
|
22
|
77
|
2013
|
85
|
43
|
128
|
1
|
1
|
2
|
6
|
2
|
8
|
53
|
22
|
75
|
16
|
10
|
26
|
9
|
9
|
18
|
86
|
Katika kuboresha
elimu hapa Wilayani miradi 10 yenye thamani ya Tsh. 721,687,326.00 imetekelezwa
kwa kipindi cha mwaka 2011/12 hadi 2012/13.
6.2.4 Vyuo
vya ufundi na elimu ya juu
Katika wilaya ya Muheza kuna chuo cha mafunzo ya udereva (Muheza Driving
school) na chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) – Kiwanda kilichopo katika
tarafa ya Bwembwera.
Pia kuna vyuo vingine viwili vya ufundi stadi katika shule 2 za Msingi
ambazo ni Mkuzi na Magila. Vituo hivi vinatoa kozi za useremala, uashi na
sayansi kimu ambapo wanafunzi wanaohitimu wanakuwa na ujuzi katika fani husika.
Aidha Wilaya imetekeleza jumla ya
miradi kumi na sita kwa mwaka 2011/12 hadi
2012/13 yenye thamani ya Ths.821,895,150.00.
6.3
SEKTA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Wilaya ina jumla ya vituo vya kutolea Huduma za
Afya 47 ikiwemo Hospitali 1 Teule. Vituo vya Afya 6 na Zahanati 41. Vituo vya
Afya 4 ni vya Serikali, kituo kimoja cha Afya kinamilikiwa na Kanisa Katoliki
na kimoja kinamilikiwa na Kampuni ya chai (EUTCO).
Zahanati 29 ni za Serikali na nyingine 12
zinamilikiwa na watu binafsi. Vilevile Wilaya
ina Chuo cha Utafiti wa magonjwa
ya binadamu na Taasisi ya Utafiti wa Malaria (NIMR).
Idadi ya Vituo
Vya kutolea Huduma za Afya na Umiliki
Kituo cha huduma
|
Idadi
|
Mmiliki
|
||
Serikali
|
Kanisa
|
Binafsi
|
||
Hospitali
|
1
|
0
|
1
|
0
|
Vituo vya Afya
|
3
|
1
|
1
|
1
|
Zahanati
|
44
|
31
|
1
|
10
|
JUMLA
|
48
|
32
|
3
|
11
|
6.3.1 Hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya Serikali:
Hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya
kutolea huduma ya Afya vya Serikali Wilayani Muheza ni nzuri.
Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya hupokea
dawa kupitia vyanzo vikuu vinne navyo ni Kupitia mgao wa Wizara kwenda MSD,
Mfuko wa pamoja wa Afya (HBF), Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na Vertical
progranne kwa dawa kama ALU, Septrine na nyinginezo.
Katika kupambana na upungufu wa dawa za
ILS Wilaya inaeendelea kuhamasisha Waganga Wafawidhi
wa vituo vya kutolea huduma kuomba na kununua dawa kupitia fedha za CHF
walizokusanya. Wilaya ya
Muheza inaendelea kununua
dawa kupitia Mfuko wa Basket Fund na kuzisambaza katika Vituo 33 vya kutolea
huduma vya serikali.
Vituo Binafsi na vya Mashirika vimeendelea
kupata mahitaji muhimu kutoka Wilayani
kama vile dawa za malaria (ALU), dawa za chanjo, dawa za TB na Ukoma, na
dawa za ARV kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
6.3.2 Magonjwa ya milipuko
Kwa kipindi cha
mwaka 2010 – 2011 Wilaya ilipata
mlipuko wa ugonjwa wa Rotavirus mwezi Aprili hadi Juni 2012 ambapo
watoto 325 chini ya miaka mitano waliugua na watoto saba walipoteza maisha. Pia
ulijitokeza mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo watu 47 waliugua na 1
kupoteza maisha.
Mwaka 2012/2013 mwezi Machi ulijitokeza
milipuko wa ugonjwa wa kuharisha uliotokana na uchafuzi wa vyanzo vya Maji
ambapo jumla ya wagonjwa 180 waliambukizwa
na hakuna kifo kilichotokea.
6.3.3 Afya ya mama na Mtoto
Katika kupunguza
vifo vya akina mama wajawazito kutoka vifo 375/100,000 kwa vizazi hai hadi
250/100,000, Wilaya imefanikiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka
281/100,000 mwaka 2010/2011 hadi vifo 232/100,000 kwa mwaka 2012/2013. Hii ni kutokana na utoaji wa huduma za Afya bure
kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. Pia Hati
punguzo 2,254 zimetolewa kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka
mitano kwa ajili ya kuwakinga na ugonjwa wa malaria.
6.3.3.1 Vifo vya akinamama wajawazito:
S/NO
|
MWAKA
|
VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO
|
1.
|
2010/2011
|
281/100,000
|
2.
|
2011/2012
|
243/100,000
|
3.
|
2012/2013
|
232/100,000
|
6.3.3.2 Chanjo
Katika
kipindi cha mwaka 2010/2011hadi 2012/2013, Idara imeendelea kutoa chanjo kwa watoto na akina mama wajawazito katika
Vituo vya kutolea huduma ya Afya pamoja na chanjo mkoba vijijini.
Mchanganuo
wa Chanjo zilizotolewa kwa watoto na
akina mama wajawazito ni kama
ifuatavyo:-
Aina ya chanjo
|
Chanjo
|
||
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
|
Lengo 8,240
|
Lengo 8683
|
Lengo 8293
|
|
BCG (Kifua Kikuu)
|
8,022 (97.3%)
|
8,188 (94.3%)
|
8,042 (97%)
|
DTPhb=Pentavalent
|
7984 (96.9%)
|
8,010 (92.2%)
|
7,988 (96.3%)
|
POLIO Kupooza
|
7891 (95.7%)
|
8,010 (92.2%)
|
7,992 (96.3%)
|
Measles
(Surua)
|
7,818 (95%)
|
7,855 (90.4%)
|
7,946 (96%)
|
TT+2
(Pepopunda)
|
8,018 (97.3%)
|
8,188 (94.3%)
|
7,904 (95.3 %)
|
PCV-13(Nimonia/Kichomi
|
-
|
-
|
7,973 (96.1%)
|
Rotavirus
|
-
|
-
|
7,962 (96%)
|
6.3.4 Mfuko wa Afya ya Jamii – CHF
Wilaya ya Muheza inaendelea kutekeleza
sera ya Mfuko wa Afya ya Jamii. Wilaya inafanya uhamasishaji kwa jamii, Vikundi
vya Ushirika, Viongozi wa Dini, watu maarufu na wadau kujiunga na mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF). Idadi ya kaya wanachama wa mfuko zimeogezeka kutoka 1,011 mwaka
2011 hadi kaya 7,730 mwaka 2013 sawa na
ongezeko la 76% kama inavyoonekana katika jedwali;
Idadi ya kaya zilizojiunga na CHF
Mwaka
|
Kaya
|
2011
|
1,011
|
2012
|
1,860
|
2013
|
7,730
|
Kuwezesha wazee wasio na uwezo kujiunga na
CHF:
Jumla
ya wazee 4,678 kati ya wazee 4617 waliolengwa wamepigwa picha kwa ajili ya
kuandaliwa vitambulisho ili wawe wanachama wa mfuko wa afya ya jamii (CHF)
hivyo kuwawezesha kupata matibabu katika vituo vyote 42 vya Serikali Wilayani.Vitambulisho 2099 vimeandaliwa na kufikishwa
kwa walengwa
6.3.5 VVU na UKIMWI
Hali ya maambukizi ya
VVU/UKIMWI imepungua kutoka 4% mwaka 2010 hadi
2.8 % mwaka 2012 kama inavyoonekana hapa chini;
Hali ya maambukizi ya VVU/UKIMWI
Mwaka
|
Waliopima
|
Kiwango cha maambukizi
|
||
Ke
|
Me
|
Jml
|
||
2010
|
9,456
|
5,668
|
15,124
|
4.0%
|
2011
|
8,242
|
7,122
|
15,364
|
3.0%
|
2012
|
4,632
|
4,040
|
8,672
|
2.8%
|
Pamoja na
Upimaji wa VVU pia Wilaya ikishirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la
Kimarekani (LEAD PROJECT) wanatoa huduma ya Dawa za kupunguza makali ya VVU
katika vituo vinne.
Aidha Wilaya imetekeleza jumla ya
miradi kumi na na miwili kwa mwaka 2011/12
hadi 2012/13 yenye thamani ya Ths. 836,607,429.00.
7.0 KUENDELEZA MAKUNDI MBALIMBALI
7.1 MAENDELEO YA WANAWAKE
Ibara ya 203 ya
Chama Tawala inasisitiza juu ya uendelezaji wa watoto, wakati Ibara 204
inasisitiza juu ya kuwahusisha wanawake katika siasa, uongozi na
modenaizesheni ya uchumi wetu kuwa na jamii iliyobora. Kwa kuzingatia
hilo Wilaya imefanya yafuatayo ;
·
Elimu ya jinsia, ujasiriamali na uongozi
imetolewa kwa washiriki 509 katika Tarafa zote 4, Lengo ni kuhakikisha kuwa
wanawake wanajengewa uwezo wa kiuchumi na demokrasia ili waweze kuteuliwa na
kuchaguliwa katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuongeza nafasi za uwakilishi
wa wanawake kwa lengo la kufikia asilimia 50.
·
Wilaya imetoa Mikopo jumla ya Tsh. 27,880,000
kwa ajili ya kuwakopesha vikundi 38 vya uzalishaji mali vya wanawake Wilayani.
Kati ya fedha hizo kiasi cha Tsh. 8,000,000 zilitolewa na Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto.. Aidha kwa Kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014
kiasi cha Tsh.70,829,000
kimeidhinishwa kwa ajili ya mfuko wa wanawake na Vijana, mikopo imetolewa Tshs
35,414,500 kwa vikundi 66 vya wanawake. Wilaya inaendelea kutoa elimu ya namna
ya kutumia mikopo ili kuboresha maisha ya wananchi wake.
7.7.1 Mikopo kupitia Mfuko wa Wanawake
Mwaka
|
Idadi ya vikundi
|
Idadi ya wanachama
|
Kiasi cha Mkopo
|
2010/11
|
38
|
190
|
8,380,000
|
2011/12
|
32
|
16
|
8,000,000
|
2012/13
|
14
|
70
|
3,800,000
|
2013/14
|
66
|
330
|
35,114,500
|
7.2 MAENDELEO YA VIJANA.
Wilaya ina jumla ya vijana 68,267 wenye umri kati
ya miaka 15 hadi 35. Zaidi ya 70% ya vijana wameajiriwa katika sekta binafsi.
Hali ya ajira kwa vijana sio nzuri kwani ajira kuu kwa wananchi wa Wilaya hii ni
kilimo, wakati mazingira ya uendeshaji kilimo bado hayajakuwa rafiki kwa
vijana. Hata hivyo sehemu kubwa ya vijana wamejiajiri katika bodaboda, viwanda
vidogo na biashara ndogondogo.
Katika harakati za kuendeleza vijana,
SACCOs ya vijana imeundwa na imesajiliwa kwa usajili namba TAR 584 ikiwa na vikundi
70 vyenye wanachama 370. Maombi ya mkopo wa Tsh. 286,300,000/= kwa ajili ya
vikundi vya vijana yamewasilishwa. Wizara ya habari Michezo, Utamaduni na
vijana bado unaendelea Pia Wilaya imetoa jumla ya Tsh. 49,114,000/=kwa
vikundi 96 kwa mchanganuo ufuatao:
7.2.1Mikopo ya Vijana
Mwaka
|
Idadi ya vikundi
|
Idadi ya wanachama
|
Kiasi cha Mkopo
|
2010/11
|
16
|
85
|
6,700,000
|
2011/12
|
0
|
0
|
0
|
2012/13
|
14
|
70
|
7,000,000
|
2013/14
|
66
|
330
|
35,114,500
|
Juhudi zaidi zinafanyika ili kuwawezesha vijana
kujiajiri na kujiongezea kipato ikiwa ni pamoja na;
·
Eneo
la ekari 100 limetengwa kijiji cha Mtiti
kwa shughuli za kilimo kwa vijana.
·
Vijana
33 wametengewa maeneo katika Skimu ya umwagiliaji ya Mashewa.
·
Vijana
75 wametengewa maeneo katika Skimu ya umwagiliaji ya Misozwe.
·
Eneo
la ekari 100 limetengwa kijiji cha Mto
wa Mbuzi kwa ajili ya kambi ya vijana na vijana 15 tayari wapo kambini.
·
Eneo
la ekari 60 limetengwa katika kijiji cha Kwemhosi kwa ajili ya shughuli za
vijana.
8.0 USAMBAZAJI UMEME
Wilaya ya Muheza
ni miongoni mwa Wilaya zinazopata umeme kutoka grid ya Taifa. Vitongoji 385
kati ya 522 vilivyoko Wilayani havijapata nishati ya umeme. Idadi ya vijiji
vyenye umeme imeongezeka kutoka 30 mwaka 2010 hadi kufikia 60 mwaka 2013. Mradi
wa usambazaji umeme kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani iliyoitwa Changamoto
ya Millenia (MCC – Project) umetekelezwa
hapa Wilayani ambapo vijiji 14 viliungiwa umeme au kuboreshwa kwa vile
vilivyokuwa tayari vina umeme, kupitia mpango huo wateja zaidi ya 40
wameunganishiwa umeme.
8.1 Ongezeko la
wananchi walioungiwa umeme
Mwaka
|
2010
|
2011
|
2012
|
2013
|
2014 (hadi Februari)
|
Idadi
|
4348
|
4662
|
4972
|
5700
|
6100
|
Ongezeko
|
314
|
310
|
728
|
400
|
8.2 Usambazaji Umeme kupitia REA
Jitihada za
kusambaza umeme katika vijiji vingine zinaendelea, ambapo Serikali kupitia
wakala wa umeme vijijini REA imetoa fedha za mradi wa kusambaza umeme katika
vijiji 30 hatua za awali zimeshaanza kufanyika ikiwa ni pamoja na wakandarasi
kutembelea vijiji hivyo kufanya tathmini. hata hivyo upatikanaji wa umeme sio
wa kiwango cha kuridhisha sana kutokana na chakavu wa miundombinu na mingine
kuzidiwa na uwezo hasa baada ya kuongezeka kwa watumiaji.
8.2 Nishati mbadala
Aidha Wilaya kupitia
shirika la TaTeDo inasisitiza matumizi ya nishati mbadala ambapo nishati ya
umeme jua inatumika kwa kiwango kikubwa hasa katika taasisi kama shule na vituo
vya kutolea huduma za Afya , kati ya mwaka 2011 hadi 2013 taasisi 15 zimewekewa
umeme mbadala ikiwemo sola 12, majiko
sanifu 2 na biogas 1)
9.0 HALI YA ULINZI NA USALAMA
Hali ya ya usalama wilayani ni ya kuridhisha, hakuna matukio makubwa
yaliyotokea ambayo yanahatarisha hali ya utulivu na amani, isipokuwa makosa ya
kawaida ya jinai, madai na usalama barabarani.
9.1 Mapambano dhidi ya Rushwa
9.1.1 Uchunguzi na mashitaka
Kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2014 jumla ya
malalamiko 153 yalifanyiwa kazi. Idara zilizolalamikiwa zaidi ni Mahakama,
Polisi, Ardhi Mabaraza ya ardhi, Afya, Maji, Misitu, Utawala, Fedha, Ukaguzi,
Ujenzi, Kilimo, Elimu, TANESCO, Vyama vya siasa na Benki ya NMB.
Mafanikio yaliyopatikana kutokana na chunguzi
dhidi ya malalamiko haya ni kama ifauatavyo;-
·
Chunguzi
dhidi ya tuhuma za vunaji haramu wa mazao ya misitu zimewezesha udhibiti wa
hujuma za mapato na kuokoa jumla ya Tsh. 8,453,000/=
·
Chunguzi
dhidi ya ukiukwaji wa madili ya kazi, taratibu na sheria zimewezesha hatua za
kinidhamu kuchukuliwa kwa watumishi 2 wa Halmasahauri (W), migogoro 2 ya ardhi
kupatiwa ufumbuzi.
·
Chunguzi
katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo zimewezesha majadala 4 ya uchunguzi kufunguliwa
na chunguzi zake bado zinaendelea.
·
Chunguzi
dhidi ya malalamiko mengine zimewezesha kesi 4 kufunguliwa mahakamani na 2 kati
ya hizo kuweza kushinda.
9.1.2 Elimu kwa Umma
Elimu juu ya rushwa, madhara yake na mustakabali
wa maendeleo ya Taifa kwa ujumla imetolewa kwa jamii, miongoni mwa makundi
yaliyopewa elimu ni pamoja na wananchi wa kawaida, asasi za kiraia, wanafunzi,
vijana, wazee, wasanii na watumishi wa umma katika idara za Elimu, Polisi,
ardhi na Serikali za Vijiji.
·
Semina
63 zimetolewa kwa jamii
·
Mikutano
ya hadhara 26 imefanyika kwa baadhi ya jamii
·
Mijadala
ya wazi 10 imefanyika
·
Klabu
30 za wapinga rushwa zimeendelea kuimarishwa katika shule za Sekondari na vyuo.
·
Klabu
27 za wapinga rushwa zimefunguliwa katika shule za msingi.
9.3.3 Udhibiti
Jumla ya dhibiti 10 zimefanyika katika kuhakikisha
sekta za umma na binafsi zinatoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia sheria,
kanuni, taratibu na mifumo inayozingatia uwazi na uwajibikaji kwa lengo la
kupunguza kero na malalamiko ya wanajamii.
Aina ya dhibiti zilizofanyika ni pamoja na;
·
Udhibiti
1 wa kusitisha utekelezaji wa zabuni iliyotolewa na Halmashauri (w)
·
Vikao
2 vya udhibiti baina ya TAKUKURU na Uongozi wa Halmashauri (w)
·
Kikao
1 cha udhibiti kati ya TAKUKURU na uongozi wa baraza la Kata Mkuzi
·
Udhibiti
1 na kikao 1 cha udhibiti kati ya TAKUKURU na Jeshi la Polisi
·
Udhibiti
1 dhidi ya utoaji haki ya dhamana katika Mahakama ya Mwanzo
·
Udhibiti
mmoja dhidi ya taratibu za utoaji wa mikopo katika Benki ya NMB
·
Udhibiti
1 dhidi ya taratibu za uunganishaji umeme kwa wateja wa TANESCO.
·
Kikao
1 cha udhibiti kati ya TAKUKURU na Chama Cha Walimu cha Kuweka na Kukopa
(UWAKAMU)
9.2 Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya
Kwa kipindi cha Januari 2013 hadi Februatri 2014
makosa 46 ya aina mbalimbali yamefanyika kama ifauatavyo;
·
Makosa
ya kupatika na bango - 20
·
Makosa
ya kupatika na mirungi - 11
·
Makosa
ya kupatika na cocaine - 1
·
Makosa
ya kupatika na pombe ya moshi -
14
Katika makosa haya jumla ya watuhumiwa 84
walikamatwa na kufikishwa mahakamani, kati ya hizo kesi 20 bado zinaendelea,
kesi zilizoshinda ni 21 na zilizoshindwa 5.
Serikali ikishirikiana na Wadau wengine inaendelea
kutoa elimu kwa jami juu ya atharai za kutumia madawa ya kulevya.
11.0 MAFANIKIO
Mheshimiwa Rais,
Wilaya yetu imefanikiwa katika maeneo yafuatayo;
·
Tumeongeza Ukusanyaji wa mapato kutoka Tshs
821,525,858 mwaka 2011/2012 hadi kufikia Tsh 1,164,934,499 mwaka 2012/2013.
·
Ukusanyaji wa mapato bila ya fedha za fidia ya
vyanzo vilivyofutwa kutoka Tsh 755,672,857 mwaka 2011/2012 hadi kufikia Tsh 855,646,270
·
Halmashauri imepata hati safi kwa miaka minne (4)
mfululizo kutoka 2009/2010 hadi 2012/2013.
·
Vituo
vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoa 29 hadi vituo 33 kwa mwaka
2012/2013.
·
Kasi
cha maambukizi ya VVU imepungua kutoka 3% hadi kufikia 2.8% mwaka 2012
·
Wilaya imefanikiwa kupunguza vifo vya akina mama
wajawazito kutoka 281/100,000 mwaka 2010/2011 hadi vifo 232/100,000 kwa
mwaka 2012/2013
·
Ufaulu
wa shule za msingi umeongezeka kutoka 29.26%
mwaka 2012 hadi 66% mwaka 2013
·
Kiwango
cha upatikanaji maji safi na ya uhakika kimeongezeka toka 56.3% mwaka
2011 hadi 62.2% mwaka 2013
12.0 CHANGAMOTO
Mheshimiwa Rais,
Kumekuwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza
1. Uhaba wa upatikanaji wa maji safi na
salama kwa ajili ya matumizi ya majumbani hususani wakati wa kiangazi maji
yanapungua sana. Hii inatokana na kuwa na chanzo cha maji cha muda mrefu
kisichokuwa na uwezo wa kutosheleza mahitaji kwa idadi ya wakazi wa Muheza kwa
sasa.
2.
Uharibifu wa mazingira unaofanywa na wachimbaji
haramu wa madini katika misitu ya asili ya Amani, unaosababisha kuharibika kwa vyanzo vya maji na bioanuwai.
3. Migogoro ya ardhi inayosababishwa na eneo
kubwa la wilaya kuwa ni mashamba yanayomilikiwa na makampuni au wawekezaji
(Private Investors) na yale ambayo yako chini ya Consolidated Holding, mashamba haya yametelekezwa kwa muda mrefu hivyo
kufanya wananchi kufanya uvamizi. Mashamba yaliyotelekezwa na wamiliki binafsi
ni Bwembwera, Kwafungo, Mtindiro na mashamba mawili ya Wilaya ambayo ni Zigi
Mimbeni na Chartur. Mashamba yaliyopo chini ya Consolodated Holding ni
Kibaranga linalosimamiwa na Bodi ya mkonge Tanzania, Geiglitz (Azimio/
Kilapura), Lewa, Sagulas na Mivumoni.
4.
Umasikini wa kipato kisichotosheleza
5. Hali ya barabara yetu itokayo Muheza
kuelekea Tarafa ya Amani haiko katika hali nzuri. Barabara ya Muheza hadi Amani
ipo chini ya uangalizi wa TANROAD.
6. Upungufu wa watumishi husuani katika kada
za Afya, walimu, Kilimo na watendaji wa Vijiji. Wilaya ina upungufu wa
watumishi 242.
13.0 UFUMBUZI WA CHANGAMOTO
1.
Kutekeleza
mpango wa muda mrefu wa kutoa maji ya mtiririko kutoka mto Zigi umbali wa
kilometa 22 hadi Muheza mjini mara baada ya kupata fedha toka Serikali Kuu. Upembuzi yakinifu umekwishafanyika, mchoro na
makisio ambayo yanafikia shilingi bilioni 13.4 yamekwishafanyika na
kuwasilishwa Wizara ya Maji, na kwakuwa hii ilikuwa ndiyo ahadi yako Mheshimiwa
Rais, uliyoitoa kwa wakazi wa wilaya ya Muheza wakati wa Kampeni za Uchaguzi
mwaka 2010, tuna matumaini kuwa mradi huu utafanikiwa.
2. Wilaya imeanza kutatua tatizo la upungufu
wa maji Muheza mjini kwa kuanzisha miradi ya muda mfupi. Miradi hiyo ni ujenzi
wa kisima kirefu Polisi Mang’enya ambao umekamilika, kununua mashine ya kuchimbia visima ambayo
taratibu za manunuzi zinaendelea na kuchimba visima 10 ambapo visima 9
vimeshachimbwa, kazi iliyobaki ni kuweka pampu ili maji yasukumwe kuingia
katika mtandao wa maji uliopo.
3. Mradi wa shughuli za kiuchumi katika eneo
la hifadhi hai ya Amani umeanzishwa kupunguza utegemezi katika mazao ya misitu
4. Mkakati wa upandaji miti umewekwa kwa kila
shule kuwa na kitalu cha miche 4000.
5. Mkoa pamoja na Wilaya imepiga marufuku
uvunaji wa misitu
6. Usimamizi na
doria ya mara kwa mara umeimarishwa.
7. Wilaya imependekeza Serikalini mashamba
kumi yabatilishwe miliki zake na kukabidhiwa kwa Halmashauri ili yaweze
kugawiwa kwa wananchi wenye shida ya ardhi. Mashamba yaliyoombewa kubatilishwa
miliki ni Sagulas, Lewa, Geiglitz (Azimio/ Kilapura), Kihuhwi, Songa ambalo limependekezwa
kumegwa, Kwafungo, Bombwera, Mivumoni, Zeneth, Kibaranga na Chartur.
8. Wilaya inaendelea kutekeleza miradi
mbalimbali inayolenga kuongeza kipato cha mwananchi mmojammoja , na hasa kuweka
msisistizo katika kuboresha mazao ya biashara ya Machungwa na viungo.
9. Wilaya imeendelea kuboresha barabara ya
Amani – Muheza kadri fedha zinavyopatina, pia kuwakumbusha Wakala wa barabara
TANROAD kila mara ili kuweaka katika mipango yake.
10. Maombi ya ajira mpya yamepelekwa Sekretarieti
ya ajira kwa ajili ya kuwapata watumishi.
14.0 HITIMISHO
Mheshimiwa Rais,
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Serikali kwa kutupatia
fedha zilizowezesha utekelezaji wa
miradi katika sekta mbalimbali katika Wilaya yetu.
Pia tunashukuru kwa msaada ambao umekuwa
ukiutoa kwa Wilaya yetu hasa katika kukabiliana na kero ya maji, migogoro ya
ardhi na shughuli za kuinua
uchumi/kutuongezea kipato.
Baada ya maelezo haya, tuko tayari
kupokea maagizo na maelekezo yatakayotuwesha kuboresha utendaji wetu wa kazi.
Kwa heshima kubwa
naomba kukukaribisha Wilayani Muheza.
Mhe. Subira Mgalu (MB)
MKUU WA WILAYA
MUHEZA
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano waTtanzania Mhe. Dkt Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
majengo ya shule moja wapo iiliyopo wilayani ya muheza.
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano waTtanzania Mhe. Dkt Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
mizinga ya nyuki ikiwa ni mradi wa ufugaji wa nyuki wilaya ya muheza.
MIRADI
ITAKAYOTEMBELEWA
NA
KUWEKEWA MAWE
YA
UZINDUZI
TAARIFA FUPI YA UJENZI WA SOKO LA
MICHUNGWANI-MUHEZA KWA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
UTANGULIZI:
Mradi huu ulianza baada ya kuongezeka kwa wafanyabiashara kwenye soko kuu
la Muheza Mjini, Wingi wa
wafanyabiashara ulisababisha kutokuwa na nafasi ndani ya soko na kupelekea
upangaji wa bidhaa chini ardhini nje ya soko kinyume na taratibu za Afya.
Hata hivyo wazo hilo limekuwa ni moja ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010 ibara ya 49 ambayo inaelekeza kuweka mazingira
mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta ya viwanda, biashara na masoko.
UTEKELEZAJI WA MRADI:
Mradi huu hadi kukamilika kwake utakuwa na majengo
makubwa 3 ambayo ni;
§ Jengo la mbogamboga na matunda,
§ Jengo la nafaka na
§ Jengo la wauzaji wa jumla
Pia kutakuwa na vibanda vya ofisi, maduka na migahawa
kuzunguka soko zima pamoja.
Ujenzi wa soko la vyakula.
Jengo la kwanza la soko limejengwa kwa awamu mbili (2) na
Wakandarasi tofauti. Hatua ya kwanza ilihusisha ujenzi wa jengo lenyewe hadi
kupaua na awamu hii ya mradi ilianza tarehe 21/06/2011 na ukakamilika tarehe
17/12/2011. Mkandarasi aitwae MASIA CONSTRUCTION & GENERAL SUPPLY LTD kwa
mkataba Na. MUH/DC/LGCDG/10/11/02 wenye thamani ya Tsh63,021,454/=
Awamu ya pili iliyohusisha umaliziaji wa soko na ujenzi
wa vizimba ilianza tarehe 24 July, 2012 na kukamilika tarehe 24 Octoba 2012,
Mkandarasi aitwae FAIR CLASS CONSTRUCTION LTD wa Morogoro kwa mkataba Na.
MUH/DC/LGCDG/2011/2012/05 wenye thamani ya Tshs.49,588,700/= hivyo thamani ya
mradi ni 112,607,154/=
Ujenzi wa soko la mboga mboga na
matunda.
Ujenzi wa mradi huu ulianza tarehe 02/10/2013 kwa mkataba
namba LGA/MDC/CTB/LGCDG/2012/2013/10
Mkandarasi aitwae COOPERATION SOLE WORKS, ujenzi kwa awamu hii
umemalizika tarehe 02/03/2014 kwa mkataba wa Tsh. 102,381, 600/=.
FAIDA ZA MRADI
§ Mradi huu umetoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo 48
kupata meza za kuuzia bidhaa, na awamu ya pili itakapokamilika utaweza kutoa
ajira kwa wafanyabiashara 72. Aidha soko hili hutoa ajira kwa wafanyabiashara
watao 2,000 kwa siku za magulio.
§ Mradi utasaidia
kupunguza urefu wa mwendo kwa wakazi wasiopungua 13,513 wa maeneo ya
Kata ya Genge na Majengo ambao awali walikuwa wanategemea kupata mahitaji yao
toka Soko Kuu la Muheza Mjini.
§ Pia mradi utasaidia kuongezea mapato kutokana na ushuru.
MIPANGO YA
BAADAYE
§ Ujenzi wa jengo la kuchambua, kufungashia na kuhifadhia matunda, mradi
huu unatarajiwa kuanza mara taratibu za manunuzi zitakapokamilika,. Mradi unategewa kuongeza thamani ya matunda
yanayozalishwa Wilayani kwa kuchambua kwa madaraja, kufungasha na kuhifadhi
katika vyumba vya baridi. Tayari Wilaya imetenga kiasi cha Tsh. 74 milioni.
§ Kujenga vibanda vitakavyozunguka soko ikihusisha eneo la
kupaki magari na maduka ya nyama. Kazi hii inatarajiwa kufanywa kwa ubia (PPP).
Ujenzi wa vibanda na maduka utakapokamilika pia utaongeza wigo wa ajira na
kipato kwa wakazi wa Muheza.
§ Kuendelea kutenga fedha za kutosha kwenye bajeti ya mwaka
2014/2015 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya soko ikiwemo vyoo, maji na
barabara
§ Taratibu za kuomba mkopo toka taasisi za fedha na
ushirikiano wa wadau binafsi (PPP) kwa ajili ya ujenzi wa soko la samaki.
HITIMISHO
Mhe. Rais,
Tunaishukuru Serikali kutupa fedha zilizowezesha
utekelezaji wa mradi huu wa soko ambao unatoa huduma kwa wananchi wa Muheza.
Pia tunakushukuru wewe binafsi kwa kuja kututembelea na kukagua shughuli zetu
za maendeleo ikiwemo mradi huu.
Mwisho tunakuomba utufungulie mradi wetu.
KARIBU SANA.
TAARIFA FUPI
YA SHULE YA SEKONDARI POTWE- MUHEZA KWA
MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
DK.
JAKAYA MRISHO KIKWETE.
1. Utangulizi
Mheshimiwa Rais
Kwa niaba ya viongozi na
wanafunzi wa shule hii ninatanguliza
shukrani zetu za dhati kwa kukubali kutenga muda wako na kuja kututembelea
haswa katika shughuli hii maalumu ya ukaguzi wa ukarabati wa madarasa sita, ujenzi
wa maabara ya sayansi, ujenzi wa vyoo matndu 8 na umaliziaji wa nyumba ya
mwalimu.
Tunayofuraha kubwa kukukaribisha hapa
Shuleni kwetu.
2. Historia
ya Shule
Shule ya Sekondari Potwe ipo katika kitongoji cha Kiwanjani katika
kijiji cha Potwe Mpirani kata ya Potwe, tarafa ya Bwembwera umbali wa kilomita
30 toka makao makuu ya Wilaya na Kilomita 8 toka barabara kuu itokayo Tanga
kwenda Segera. Shule ina eneo la ekari 38.9.
Shule hii ni ya kutwa na
mchanganyiko na ina kidato cha kwanza hadi cha nne (I- IV). Shule ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa
na vyumba viwili (2) vya madarasa na jumla ya wanafunzi 59, waalimu watatu na wafanyakazi wengine wawili.
Shule ilipata usajili wa namba S.2012 na kituo cha mtihani wa Baraza S.2255.
Kwa sasa shule ina idadi ya vyumba kumi (10) vya madarasa na ofisi tatu. Idadi
ya wanafunzi ni 249 kati yao wavulana ni 129 na wasichana 120, ikiwa na waalimu
19 (wanaume 14 na wanawake 5) ambao wamepangiwa mnamo mwaka 2013 baada ya kuwa
na upungufu kwa muda mrefu. Shule inafanya
mitihani ya Mock na Taifa kwa kidato cha pili na cha nne na matokeo ni ya
wastani.
3. UTEKELEZAJI
WA MRADI.
Ujenzi ulianza rasmi tarehe
30/07/2013 ukihusisha ujenzi wa maabara
moja itakayo tumika katika masomo matatu yaani
Fizikia, Baiolojia na Kemia, ujenzi wa choo cha wanafunzi matundu nane
(8). Ukarabati wa madarasa sita na ofisi mbili za walimu na umaliziaji wa
nyumba moja ya mkuu wa shule, kazi hii imefanywa na Mkandarasi wa kampuni ya Kimataifa
ya MOTOSACHI ya Dar es salaamu, iliyo
ingia mkataba namba LGA / MUH/DC/ED 2012/2013/02. Wenye thamani ya Tsh.
217,509,800.
4. Faida
za mradi.
Mradi huu umekuwa na manufaa kishule,
kijamii na kitaifa kwa ujumla, ikiwemo;
·
Wanafunzi
watapata fursa ya kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo ambayo huwa ni vigumu
kueleweka bila mafunzo kwa vitendo.
§
Ongezeko
la ufaulu kwa masomo ya sayansi kutaipa shule fursa ya kutoa watalamu wa
sayansi katika Taifa .
Hakika mradi umepokelewa kwa furaha kama mkombozi kwa wanajamii, pia kwa sasa
tunaendelea na ujenzi wa maabara zingine mbili kwa nguvu za wanakijiji hadi sasa mradi huo umefika hatua ya jamvi.
5. Changamoto
Changamoto zinazo ikabili shule ni pamoja na:-
§
Uhaba
wa nyumba za walimu, kwani kuna nyumba mbili pekee za waalimu
§
Ukosefu
wa umeme na maji suala linalowapelekea wanafunzi kutafuta huduma ya maji umbali
mrefu.
§
Upungufu
wa walimu wa Sayansi ambapo wapo watatu na mwalimu wa hisabati hakuna kabisa.
§
Ukosefu
wa mabweni ya wanafunzi hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wengi wanatoka vijiji
vya mbali.
§
Ukosefu
wa jengo la utawala , Bwalo la chakula na jiko.
6. Mikakati
ya kukabiliana na changamoto.
·
Halmashauri
kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miuondombinu ya shule pia
kuhamasisha wananchi kuchangia katika shughuli za ujenzi wa miundombinu.
·
Halmashauri
kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kama World Vision kuomba
kusogeza huduma ya maji katika maeneo ya shule na vijiji vya jirani.
·
Kuendelea
kupanga waalimu wa sayansi kulingana na mgao wa waalimu kwa mwezi March, 2014 kutoka
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
MWISHO
Tunaishukuru Serikali kutupa fedha zilizowezesha
utekelezaji wa mradi huu wa ukamilishaji wa miundombinu ya shule. Pia
tunakushukuru wewe binafsi kwa kuja kututembelea.
Kwa heshima tunaomba ukague shughuli zilizofanywa katika
uboreshaji wa miundombinu ya shule yetu.
KARIBU SANA.
TAARIFA YA MRADI WA
MAJI KATIKA KIJIJI CHA KWEMHOSI - MUHEZA KWA MHESHIMIWA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
DK. JAKAYA MRISHO
KIKWETE.
UTANGULIZI.
Katika
kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010- 2015 ibara ya 86 Halmashauri
ya Wilaya ya Muheza imetekeleza mradi wa
maji katika kijiji cha Kwemhosi ili kupunguza kero ya maji kwa wananchi wa
kijiji hicho.
UTEKELEZAJI WA MRADI
Kijiji
cha Kwemhosi ni moja kati ya vijiji kumi vilivyochaguliwa na Halmashauri ya
Wilaya Muheza ili kutekeleza mradi wa Maji kupitia Mpango wa WSDP (Water Sector
Development Program).
Mradi
wa Maji Katika Kijiji cha Kwemhosi umejengwa na Mkandarasi aitwaye SERICO COMPANY LTD ya Dar Es Salaam
akisimamiwa na Kampuni ya Ushauri ya COWI
TANZANIA kwa mkataba Na. LGA/MUH//WSD/2012/2013/01. Mradi huu ulikuwa wa
kipindi cha Miezi sita kuanzia tarehe 28 February, 2013 hadi tarehe 28 August,
2013.
Gharama
za Mradi huu hadi kukamilika kwake ni kiasi cha Tsh. 224,996,000.00
Kazi
zilizofanyika katika mradi huu ni kama ifuatavyo:-
1.
Kujenga
tank la lita 90,000
2. Kujenga
fence kuzunguka eneo la tank
3. Kujenga
vituo 12 vya kuchotea maji
4. Kuchimba
mtaro na kulaza bomba kiasi cha kilometa
7.17
5. Kujenga
Manhole chemba 30
6. Kuweka
alama 25 sehemu zilipopita bomba
(Markers)
Kabla ya
mradi huu wakazi wa kijiji hiki walikuwa wanapata maji kutoka katika kisima
kirefu kilichochimbwa na Halmashauri kupitia program ya Maji Vijijini na
walikuwa wanatembea umbali wa kilometa 1 kufuata huduma ya maji.
Mradi huu
hadi kukamilika una uwezo wa kutoa lita 90,000 za maji kwa siku na unahudumia
jumla ya wakazi 1,604 kutoka katika kijiji cha Kwemhosi.
HITIMISHO
Tunaishukuru
Serikali kutupatia fedha zilizowezesha utekelezaji wa mradi huu wa maji ambao unatoa huduma kwa wananchi wa
kijiji cha Kwemhosi. Pia tunakushukuru wewe binafsi kwa kuja kututembelea na
kukagua shughuli zetu za maendeleo ikiwemo mradi huu.
Mwisho tunakuomba utuzindulie mradi wetu.
KARIBU SANA
TAARIFA YA UNUNUZI
WA MTAMBO WA KUCHIMBA VISIMA VIREFU - MUHEZA KWA MHESHIMIWA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
1.
UTANGULIZI:
Mheshimiwa Rais.
Katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
-2015 ibara ya 86 inaelekeza kuongeza
upatikanji wa huduma ya maji salama kufikia asilimia 65 vijijini na mijini
asilimia 75 ifikapo mwaka 2015. Wilaya ya Muheza imejipanga vizuri kukabiliana
na tatizo la maji lililopo Muheza.
Uongozi wa
Wilaya kupitia Baraza la Madiwani la
Halmashauri liliazimia kununua mashine ya
kuchimbia visima vya maji kwa kutumia fedha zake za mapato ya ndani.
Mtambo huo unafahamika kwa jina la PAT – DRILL 401 AND COMPRESSOR ATLAS
COPCO XAHS 186] wenye
uwezo wa kuchimba visima virefu hadi
kufikia mita 150 – 200 kwa kiasi kidogo cha dizeli (40) na kupasua miamba.
1. UTEKELEZAJI
WA MRADI
Mchakato wa
ununuzi wa mashine ya kuchimba visima virefu (PAT – DRILL 401 AND COMPRESSOR ATLAS COPCO XAHS 186]
ulianza tarehe 04.06.2013 ambapo
Halmashauri ilifanya mawasiliano na PAT – DRILL 401 AND COMPRESSOR ATLAS COPCO
XAHS 186 iliyopo Nairobi Kenya. Baada ya kuona gharama zake ziko juu. Wilaya iliamua kufuatilia Gharama za
Ununuzi wa Mtambo huo kwa Makao Makuu ya Kampuni
ya “PROMOTION OF APPROPRIATE TECHNOLOGY CO. LTD, BANGKOK, THAILAND” na kugundua
kuwa gharama za ununuzi ni USD 137,835.63 sawa na Tshs 227,428,789.5 ikiwa kuna
tofauti ya USD 56,541.7 sawa na Tshs 93,293,805 kwa kufanya manunuzi hayo
Kenya. Gharama ya ununuzi wa mtambo kutoka Bangkok Thailand zinahusisha pia
gharama za bima ya mtambo na usafirishaji wa mtambo mpaka Bandari ya Dar-
Es-Salaam [CIF].
- MCHAKATO WA MALIPO.
Kwa minaajili ya
kujihakikishia usalama wa fedha za Halmashauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji iliwasiliana na Benki ya
CRDB ili iweze kufanya malipo kwa niaba yake kupitia “Documentary Credit No.
CRDB13ILCxxx”.
Hata hivyo, kabla ya mashine hiyo kusafirishwa na
kuingia Tanzania, ilikaguliwa, yaani umefanyiwa “Pre Shipment Verification of
Conformity - PVoC” ambapo Mamlaka ya Viwango Tanzania - TBS wana wakala nchini
Thailand – [SGS Thailand]. Hivyo basi gharama za mtambo ni Tsh. 249,140,622.54 kama ifuatavyo; Gharama ya ununuzi wa
mtambo Tsh. 231,522,100.00, Gharama ya
Ukaguzi, Bima, Ushuru wa forodha, utoaji bandarini, usafirishaji Tanga – Muheza
ni Tsh. 17, 612,522.54.
3. USAFIRISHAJI
Tarehe
23/01/2014 mtambo umesafirishwa kutoka Bandari ya Bangkok Thailand kuelekea
Bandari ya Dar-Es-Salaam – Tanzania.
Hata hivyo baada
ya kupokea “Bill of ladding“ Halmashauri iliweza kufanya mawasiliano na Wakala
wa Meli iliyosafirisha Mtambo huo na kupata taarifa kwamba meli hiyo itapita
bandari ya Tanga tarehe 27/02/2014 mpaka tarehe 2/03/2014 na kutuwezesha
kufanya maombi ya kubadilisha Bandari ya kupokelea mtambo. Tarehe 27/02/2014 mtambo
huo ulishushwa bandari ya Tanga.
4. FAIDA ZA MRADI.
·
Kuongeza
na kuboresha huduma ya upatikanaji maji katika Wilaya
·
kupunguza gharama za uchimbaji wa visima hapa Wilayani.
·
Kuongeza
wigo wa ajira kwa wakazi wa Muheza
·
Kuongeza mapato ya Halmashauri kutokana na kazi ya
kuchimbia visima endapo mtambo utakodishwa.
5. MIPANGO YA BAADAYE
Hili
kuhakikisha Matumizi ya Mtambo huu yanakuwa endelevu , Halmashauri ya Wilaya
Muheza imepanga kufanya yafuatayo:
·
Kutoa mafunzo kwa wataalam wa Halmashauri ambapo Mtaalam
kutoka Kampuni ya Pat-drill Kenya atatoa mafunzo.
·
Kutunga sheria ndogo za uendeshaji wa mtambo ambapo
Kijiji/Eneo lolote kitakalochimbwa kisima wananchi watachangia kiwango
kitakachopitishwa na Halmashauri ili Mtambo huu uweze kujiendesha wenyewe.
·
Kuunda Kamati ya uendeshaji
MWISHO
Tunakushukuru kwa kuja kututembelea na kukagua miradi ya
maendeleo. Kwa heshima tunaomba ukabidhi mtambo wa kuchimba visima viongozi wa
Wilaya.
KARIBU SANA
TAARIFA
FUPI YA UFUGAJI NYUKI KWA VIJANA
- MUHEZA KWA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
DK.
JAKAYA MRISHO KIKWETE.
UTANGULIZI.
Halmashauri
ya Wilaya ya Muheza imeazimia kutumia fursa ya Ufugaji Nyuki
kwa lengo la Kuboresha na Kuongeza Kipato kwa Vijana. Ili kutimiza azma hiyo,
mkakati maalum wenye lengo la kuhamasisha, kuratibu na kusimamia shughuli hiyo
umeanzishwa rasmi. Mkakati huo unafahamika kama“Mpango wa Ufugaji Nyuki kwa Vijana”ambao kwa kifupi unaitwa “MUNVI”.
MALENGO.
Mpango
wa Ufugaji Nyuki kwa Vijana unalenga kutoa hamasa kwa vijana mbalimbali waliopo
katika Wilaya ya Muheza, hasa kwenye maeneo yenye fursa nzuri kwa Ufugaji wa
Nyuki. Kwa kuanzia, vijana wapatao 100 watawezeshwa chini ya mpango huu ili
waweze kujiajiri kupitia Sekta ya Ufugaji Nyuki katika vijiji 10, ambavyo ni
Vijiji vya Kazita , IBC Msasa, Mgambo Miembeni, Kimbo, Mashewa, Sakale,
Kilongo, Mto wa Mbuzi, Mlingano na Mhamba .
Mpango
huu utawajengea uwezo vijana hawa kwa kuwapa Mafunzo ya Mbinu Bora na za Kisasa
za Ufugaji wa Nyuki. Mpango unategemea pia kuwapa vijana vifaa muhimu kama
Mizinga ya Kisasa 5000 na Mavazi ya Kinga za Nyuki jozi 500.
Vijana
wataweza kuzalisha mazao ya Nyuki kama Asali na Nta, kuyauza na kujipatia
Kipato. Pia kwa njia hii watakuwa wanachangia na kuhamasika kutunza Mazingira
kwa kuwa Nyuki ni Baioanuai rafiki wa Mazingira. Vijiji vinasaidia kutenga
maeneo kwa ajili ya vijana hawa kuweka/kutundika mizinga yao.
UTEKELEZAJI
Kwa
mwaka 2013/14, mpango huu umeanza utekelezaji wake katikaTarafa ya Amani ambako
unafanya kazi na Umoja wa Wafugaji Nyuki Amani, “UWANA”.Umoja huu una jumla ya
wanachama 45, wavulana 30 na wasichana 15. Umoja ulianza na Mizinga ipatayo 20
mnamo mwaka 2009 na kwa sasa kuna Mizinga ipatayo 133. Lengo la umoja huu ni
kufikisha idadi ya Mizinga 2,000 ifikapo mwaka 2020.
Mpango
wa Ufugaji Nyuki kwa Vijana unatoa Mizinga ya Kisasa 100 yenye thamani ya Tsh.
6,500,000/= kwa Umoja wa Wafugaji Nyuki Amani ili kuchangia katika juhudi zao
za uzalishaji wa asali kwa lengo la kujiongezea kipato.
MAFANIKIO
Umoja
huu kwa sasa unauwezo wa kuzalisha Lita 600 zaAsali kwa mwaka, na huingiza
fedha kiasi cha Shilingi Milioni Nne na
Laki Mbili kwa mwaka (Tshs 4,200,000/=).
CHANGAMOTO
- Kikundi kinakabiliwa na uhaba wa vifaa na vitendea kazi muhimu kama vile:-Mizinga, Mavazi ya Kinga, Zana za Mizinga, Mitambo ya Kurinia Asali, Vifaa vya Kuhifadhi na Kufungashia Asali.
- Kuwepo kwa wadudu waharibifu (wanasumbua nyuki)
- Ukosefu wa Elimu juu ya ufugaji wa nyuki.
MIKAKATI YA KUKABILIANA
NA CHANGAMOTO
- Kuendelea kuwapatia vifaa na vitendea kazi muhimu kadiri uwezo utakavyoruhusu.
- Kutoa elimu ya kupambana na wadudu waharibifu na wasumbufu kwa Nyuki ikiwa ni pamoja na kusaidia dawa za kudhibiti wadudu hao.
- Kutoa elimu ya Ufugaji Bora wa Nyuki kwa njia ya kisasa kwa lengo la kuzalisha Asali na Mazao mengine ya Nyuki kibiashara.
HITIMISHO
Mhe Rais
Tunaishukuru Serikali kutupa fedha zilizowezesha
utekelezaji wa mpango huu. Pia tunakushukuru wewe binafsi kwa kuja kututembelea
na kukagua shughuli zetu za maendeleo ikiwemo kukabidhi mizinga ya kisasa 100
kwa Umoja wa wafugaji nyuki Amani.
Mwisho tunakuomba ukabidhi mizinga ya nyuki.
KARIBU SANA.
0 comments:
Post a Comment